Kwa nini Gloria Muliro amekuwa kimya kwenye muziki

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Gloria Muliro amejifungua mtoto wake wa kwanza.

Muhtasari

•"Wale wanawake ambao wametajwa. Gloria hivi majuzi alipokea mtoto, wakati Eunice anatunza familia yake," Lady Bee alisema 

•Mwezi Novemba mwaka jana, Muliro alisherehekea ukumbusho wa harusi yake na mumewe Evans Sabwami.

Evans Sabwami and Gloria Muliro
Image: HISANI

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Gloria Muliro amejifungua mtoto wake wa kwanza.

Mwimbaji mwenzake Bernice Mugo, almaarufu Lady Bee, alifichua habari hizo wakati wa misa ya wafu ya Ilagosa Wa Ilagosa mnamo Ijumaa.

Lady Bee alikuwa akieleza ni kwa nini baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili ilibidi waache kazi zao za muziki.

"Wale wanawake ambao wametajwa. Gloria hivi majuzi alipokea mtoto, wakati Eunice anatunza familia yake," alisema na kuongeza kuwa familia ndiyo kitu cha kwanza.

Aliongeza kuwa watu wanapaswa pia kuangalia wale wasanii ambao wanafanya vizuri baada ya kugura tasnia ya kidunia.

"Size 8 pia alikuja na Mungu ametubariki. Nilikuwa nikivuta bangi na injili iliniokoa," alisema.

"Huduma si muziki bali ni nguvu ya wokovu wa Mungu."

Mwezi Novemba mwaka jana, Muliro alisherehekea ukumbusho wa harusi yake na mumewe Evans Sabwami.

Gloria alizamia kwenye mtandao wa kijamii na kumtaja mume wake kama rafiki yake mkubwa.

"Sikukuu ya Furaha zaidi, rafiki yangu bora, mpenzi wangu wa moshene, mume wangu. Upendo wako ni zawadi ninayofungua kila siku. Hapa ni kwako, hapa ni kwetu, hapa ni kwa miaka mingi ya furaha pamoja. Heri ya kumbukumbu ya miaka, hun! Ninakupenda."

Wawili hao walifunga ndoa ya kupendeza jijini New York, Marekani mnamo Oktoba 2021, miaka sita baada ya talaka yake na mtayarishaji wa muziki Eric Omba.

Mwimbaji huyu alishiriki picha yake na mumewe, akinukuu, "Hatimaye hatimaye. Harusi yangu ya vuli New York."