Dadake Diamond amenizuia kuona mtoto, asema aliyekuwa mumewe

Petit na Esma wana mtoto wa kike anayeitwa Taraj.

Muhtasari

• Petit Man Wakuache amedai kuwa aliyekuwa mke wake Esma, dadake Diamond amemzuia kuona binti yake.

Mjasiriamali Esma Khan, dada mkubwa msanii Diamond Platnumz
Mjasiriamali Esma Khan, dada mkubwa msanii Diamond Platnumz
Image: Instagram

Aliyekuwa shemeji wa Diamond Platnumz, Petit Man Wakuache amedai kuwa aliyekuwa mke wake Esma, dadake Diamond amemzuia kuona binti yake.

Petit na Esma wana mtoto wa kike anayeitwa Taraj.

Mfanyabiashara huyo alichapisha ujumbe mrefu kwenye Instagram kuhusu hisia zake dhidi ya Esma na Taraj.

Alisema Esma anakaa na kumlea binti yao pekee.

Petit alisema Esma kumnyima haki yake kama baba ni kuvunja sheria.

"Juzi nilijaribu kupeleka zawadi za mtoto wangu shuleni kwake lakini niliambiwa kuwa kuna maagizo maalum kutoka juu kuwa siwezi kumuona," aliandika kwenye Instagram.

“Nimezipokea na nimeziweka nyumbani siku akija kuziona stori itaendelea...)

Petite ana mtoto mwingine, mvulana na mke wake wa sasa

Alisema bintiye na mwanawe hawawezi kujuana kwa sababu ya kutokuwepo kwake.