Mwanadada ailiyegonga vichwa vya habari baada ya kuonekana na wasanii Harmonize na Rayvanny katika vipindi na sehemu tofauti, Feza Kessy ameibuka na mapya kuhusu mwanamume wa ndoto zake.
Kessy anasema kwamba anatamani kumpata mwanamume wa kipekee ambaye kazi yake itakuwa kumwaga pesa katika maisha ya mwanadada huyo, kila sekunda, kila siku.
Mrembo huyo ambaye alifana kama vixen wa video kwenye ngoma ya ‘Wote’ ya msanii Harmonize anadai kwamba angependa kupata mwanamume ambaye iwapo Kessy hatomuomba pesa basi mwanamume huyo ana kila haki ya kumgombanisha ni kwa nini hataki kumuomba pesa.
“Nataka mpenzi ambaye nisipomuomba hela ananigombeza,” Kessy alisema.
Kauli hii yake ilionekana kama kinaya kwani kwa kawaida, angeshauri wanawake kutopenda hela katika uhusiano wa kimapenzi.
Watu wengi walitoa maoni tofauti, baadhi wakimwambia kwamba na uchumi huu wanaume nao wamechanuka hawatoi hela ovyo ovyo kisa mapenzi, baadhi pia wakisema wanaume kama hao hawapo hai katika enzi hii.
“Wapo wengi tu, wanaitwa wapenzi watazamaji,” Catherine Njarika alimwambia.
“Wanaume wa sampuli hiyo walishakufa wote katika vita ya maji maji,” Shamsa Ford alimtania.
Wengine walisema siku hizi wanaume wengi wanatafuta mwanamke ambaye wakimpa hela anakataa wakati yeye anataka mwanamume kumpa hela mfululizo.
Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii walidhani kabisa Kessy ndiye windo jipya la Harmonize baada ya kuonekana katika hali ya mahaba makubwa kwenye video ya Wote. Kessy na Harmonize kwenye video hiyo walionekana wakiwa sehemu kama ya bafu hivi wote wakiwa nusu uchi upande wa juu – Si Harmonize alikuwa na fulana wala Kessy kuwa na nguo yoyote ya kusitiri kifua chake. Wote walibanana wakipiga mswaki.
Wiki tatu baadae, mrembo huyo pia alionekana kaketi kwenye kochi na Rayvanny msanii huyo akimchezea gitaa, jambo ambalo lilizua hisia kuwa huenda kama si ngoma walikuwa wanaratibu basi Rayvanny alikuwa anajaribu kuingia kwenye anga ya Harmonize.
Ukweli ni kwamba mwanadada huyo hakujitokeza wazi kukiri au kukanusha uvumi wa kutoka kimapenzi na wasanii hao wawili.