(VIDEO)Mcheshi kutoka Eldoret atembea uchi baada ya Man U kupewa kichapo na Liverpool

Wakati fulani, anavua jezi na kutembea uchi tu kufunikwa na diapers ya watu wazima.

Muhtasari
  • Alisema alichukua hatua hiyo kama njia ya kutimiza ahadi yake na kuendelea kuwa mwaminifu kwa Manchester United
Gogo Small
Image: screen grab

Mcheshi maarufu wa Kalenjin amezua tafrani mtandaoni baada ya kutembea uchi katika mitaa ya mji wa Eldoret saa chache baada ya Manchester United kucharazwa vibaya na Liverpool.

Mchekeshaji huyo anayeishi Eldoret kwa jina la kisanii Gogo Small, Jumapili, aliahidi kutembea uchi katika mitaa ya jiji hilo iwapo Liverpool wataifunga united.

Na kweli kwa ahadi yake, Gogo aliingia mitaani Jumatatu mchana akiwa amevalia jezi ya united.

Wakati fulani, anavua jezi na kutembea uchi tu kufunikwa na diapers ya watu wazima.

"Mshabiki wa Manchester tupatane Eldoret CBD kesho tutembeeni uchi pamoja,"Ujumbe wake wa Jumapili ulisoma.

Ni kitendo ambacho kimewafanya watu wengi kufurahishwa mtandaoni, huku baadhi ya wanamtandao wakijitokeza kumkosoa.

Alisema alichukua hatua hiyo kama njia ya kutimiza ahadi yake na kuendelea kuwa mwaminifu kwa Manchester United

Liverpool ilishinda man u kwa mabao 7-0 katika mechi ya kuburudisha iliyochezwa kwenye uwanja wa Anfield Jumapili jioni.

HII HAPA VIDEO YA MCHESHI HUYO;

Loyalty Manchester United 🙏🙏🙏🙏 Betika

Posted by Gogo Small on Monday, March 6, 2023