Vita vya maneno kati ya wanablogu wa YouTube Diana Marua na Andrew Kibe vinaonekana kutopata mwafaka hivi karibuni, hii ni baada ya Marua kumjibu vikali Kibe, saa chache baada ya mwanablogu huyo anayeishi Marekani kumkejeli mitandaoni.
Kupitia Instagram yake, Marua aliibua picha ya zamani ya Kibe akiwa na mwanamke ambaye alisema anadhaniwa kuwa alikuwa mpenzi wake kabla ya kuachana.
Marua alisema kwamba anahisi mwanamke huyo anayetajwa kumtenda vibaya sana Kibe ndiye chanzo kikubwa cha Kibe kutoona zuri katika ndoa au mapenzi, kwani anatumia muda mwingi kukejeli wapenzi.
“Inakuwaje Kifee awe anachukia watu wote walio kwenye Ndoa??? hii ni Kawaida kweli???” Maru aliuliza.
Aliwataka mashabiki wake kuungana naye ili kumtafuta mwanadada huyo anayedhaniwa kuwa mpenzi wa Kibe na kumrudisha kwa mwanablogu huyo ilia pate kuona thamani katika ndoa, huku akisema kwamba mwisho wa siku atamalizia kujitoa uhai iwapo hawatamtafutia mke.
“Swali la siku : nani aliumiza Andrew kifeiliaa??? Ikiwa huyu Bibi kwenye picha hii ndiye aliyevunjika moyo huyu mtangazaji wa zamani wa Radio aliyefeli ... tunaomba amrudie kwa sababu sisi wengine tunaumia juu ya hiyo Talaka. Tafadhali tuje wote pamoja na tumsihi huyu mwanadada anayedhaniwa kuwa mke wa zamani wa Kibe ili arudi kwake. Kifee amechoka kujilipua, sasa atajinyonga.”
Hata hivyo, baadhi walihisi si hatua nzuri kuivuta picha ya mwanamke huyo kwenye ugomvi wao na Kibe na kumtaka kutochukua mkondo huo.
“Kwa kweli natamani usilazimike kumleta mwanamke katika hili. Msichana huyo labda anaishi maisha yake ya utulivu. Kulea watoto wake au kitu. Yeye ni mwanamke kama wewe. Hajafanya kosa lolote. Hata hajakukosea jamani. Sijui kwanini umemuingiza kwa vita vyako na Kibe,” mmoja alimwambia.
“Achana na mke wake wa zamani katika hili. Kibe ni mtu mdogo asiyebadilika eith hana sifa za kukomboa kama binadamu lakini sioni maana ya kumvuta ex wake ambaye pengine anachukia wake pia kwenye wazimu wake,” Missi K aliandika.