Msiseme vile nimeiba mabwana hio haibambi-Ujumbe wa Karen Nyamu uliozua gumzo mitandaoni

Awali waandamanaji waandalizi wa maandamano walipanga kuwa maandamano hayo yangeelekea katika Ikulu ya rais

Muhtasari
  • Aidha mwanasiasa huyo amewafahamisha kuwa hajafurahishwa na jinsi baadhi ya wanamitandao wengi wanasema kwamba amekuwa akiwanyakua waume wa wenyewe.
Karen Nyamu ataniana na Wakisii Facebook.
Karen Nyamu ataniana na Wakisii Facebook.
Image: Facebook

Karen Nyamu ni miongoni mwa wafuasi sugu wa Rais Ruto, huku akizungumzia maandamano ya Azimio, Karen amewaruhusu wafuasi wake kutoa maoni yeyote kuhusu maandamano hayo.

Aidha mwanasiasa huyo amewafahamisha kuwa hajafurahishwa na jinsi baadhi ya wanamitandao wengi wanasema kwamba amekuwa akiwanyakua waume wa wenyewe.

Kwa muda sasa Nyamu amekuwa akivuma mitandaoni baada ya kutangaa uhusiano wake na msanii wa mugithi Samidoh.

"Kuna maandamano ingine ama ni hii tu? Raila is finished! odm uwanja ni wenyu sasa kwa comments, na msiseme vile nimeiba mabwana pls hio haibambi,"Karen Aliandika.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alijiunga na waandamanaji mjini Nairobi wanaopinga kupanda kwa garama ya maisha.

Akishangiliwa na umati wa wandamanaji waliokuwa wakipaza sauti, 'Unga!, Unga!, Unga!...'' Bw Odinga amesema maandamano yataendelea hadi garama ya maisha itakaposhuka.

Haijajulikana msafara wa bw Odinga unaelekea wapi, huku baadhi ya barabara za kuingia katikati mwa mji zikiwa zimefungwa na maafisa wa usalama.

Raila amesema kuwa maandamano ya aina hiyo yataendelea kufanyika kila Jumatatu, na ametoa wito wa kuachiliwa huru kwa viongozi wa upinzani waliokamatwa.

Awali waandamanaji waandalizi wa maandamano walipanga kuwa maandamano hayo yangeelekea katika Ikulu ya rais kuwasilisha malalamiko yao kwa Rais William Ruto. Hata hivyo jaribio la kufika Ikulu limekwama baada ya barabara ya Ikulu kufungwa.