logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mimba ni baraka isiyofichika, popote utaenda kila mtu atajua uko na baraka - Nyce Wanjeri

Wanjeri na Leting walitangaza ujauzito wao wiki tano zilizopita.

image
na Davis Ojiambo

Burudani27 March 2023 - 07:17

Muhtasari


  • β€’ Wapenzi hao wanatarajia mtoto wa pili pamoja hivi karibuni.
Nyce Wanjeri akifurahia safari ya ujauzito wake na mpenziwe Leting.

Nyce wa Njeri na mpenzi wake Galvin Leting wanazidi kutamba na ujauzito wao, woki tano baada ya kufichua kutarajia mtoto pamoja.

Wa Njeri alipakia picha ya pamoja na mpenzi wake na kusema kwamba ujauzito huo si suala la kuficha kwani Mungu mwenyewe aliamua kwamba ni sharti uonekane na kila mtu, kila mahali aendapo.

Kulingana na mwigizaji huyo, ujauzito wake ni kama Baraka ambapo haifichiki hata kidogo.

“Hii ni baraka moja yenye Mungu alikataa kuficha πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯..... Alisema popote utaenda kila MTU anajua uko Na Baraka,” Nyce wa Njeri alisema.

Msanii huyo aliwatakia wafuasi wake kheri na Baraka ya Mungu kuwatiririkia wazi wazi kama ambavyo mimba yake inaonekana wazi pasi na kufichika.

“Maombi yako yajibiwe hadharani ndio Mungu aoneshe umaarufu wake Na wewe πŸ™. Mwamini Mungu atakuvusha katika hayo yote.... Ana uwezo kuliko kitu kingine chochote πŸ™. Wewe ni baraka katika jina la Yesu... Amina?” wa Njeri alitoa himizo.

Wiki tano zilizopita, wapenzi hao walitangaza ujauzito wao ambapo Wa Njeri anatarajia mtoto wa pili. Walitangaza ujauzito wao kupitia video ya wimbo waliouita ‘Kwako Nyumbani’

Baadaye, mwigizaji huyo wa zamani wa Auntie Boss alishiriki picha ya mimba yake kwenye Instagram akiwa kando ya mpenzi wake. Picha hizo zilivutia jumbe nyingi za pongezi kutoka kwa mashabiki wao mtandaoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved