Mwigizaji mkongwe wa bongo fleva Wema Sepetu ni mjamzito hatimaye, mpenzi wake mpya Whozu amefunguka ukweli wote kupitia Instagram yake.
Kwa muda wa miezi miwili hivi, wapenzi hao wamekuwa wakiashiria kuwa huenda hatimaye wamefanikiwa kupata ujauzito, haswa kwa Sepetu ambaye amekuwa akionesha uchu wa kupata mtoto wake, baada ya majaribio kadhaa kufeli.
Whozu alipakia picha ya pamoja akiwa na Sepetu wakiwa wamevalia kiislamu na kuwatakia ndugu Waislamu mfungo wa Ramadan wenye fanaka.
Picha hiyo hiyo aliichapisha kwenye instastory yake na kuandika maneno ya kudokeza kwamba suala la kutarajia mtoto si ndoto tena bali ni kitu kipo, ila wasichokijua mpaka sasa ni jinsia tu ya mtoto.
Hata hivyo, Whozu mwenye matumaini makubwa ya kuitwa baba alisema maombi yake ni mtoto huyo kuwa wa kiume.
“Na katoto ketu kawe ka kiume inshaallah,” Whozu aliandika kwenye picha hiyo.
Kwenye picha hiyo, Sepetu amevalia dera na kwa mbali anaonekana kama kitumbo kimechomoza lakini wengi bado walionekana kutoamini na maneno hayo ya Whozu wakisema kuwa zimekuwa ndizo kauli kutoka kwa Sepetu siku nenda rudi akijiaminisha kuwa atapata mtoto kwa miaka mingi tu bila mafanikio.
“Katika yale maajabu saba ya dunia, Wema kupata mtoto litakuwa la nane,” mmoja kwa jina Frey Scoot alisema.
Wengine walimuombea Sepetu angalau kujibiwa ombi lake la kupata mtoto, kwani amekuwa akionesha nia kwa muda mrefu.
“Itakuwa ni kweli, jana niliwaona kliniki,” mwingine alisema.
“Eee Mungu sikio lako siyo zito...wema apate mtoto,” mwingine alitia dua.
Wiki mbili zilizopita baada ya Sepetu kukanusha madai kuwa alikuwa mjamzito, watu mbalimbali waigizaji wenzake waliopata watoto akiwemo Jacqueline Wolper walijitolea na kuweka nadhiri naye kwamba ikitokea amepata ujauzito, yeye atajitolea kumhudumia kwa kila kitu, huku Sepetu akiwa ndani kama mwanamwali asiyefanay kitu chochote.