logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Abel Mutua anunua gari jipya baada ya kutumia gari yake ya awali kwa mika minne.

Mwanafilamu Abel Mutua anunua gari jipya la Land Rover Discovery 4.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 May 2023 - 08:20

Muhtasari


  • • Muigizaji Abel Mutua alizindua gari lake jipya la kifahari, Land Rover Discovery 4,
  • • Mutua aliaga gari lake aina ya Mercedes Benz na kukumbatia gari jipya aina ya Land Rover Discovery 4.
Abel Mutua

Mwanafilamu maarufu Abel Mutua amenunua gari jipya aina ya Land Rover Discovery 4.

Abel amekuwa akiendesha gari  aina ya Mercedes Benz E250 ambalo amemiliki  kwa Zaidi ya miaka .

Katika video iliyoichapishwa kwenye akaunti ya Instagram ya rafiki yake Eddie Butita, Abel alionekana mwenye furaha tele huku akikagua gari hilo.

Katika video hiyo Eddie Butita anaonekana kumkejeli rafiki wao wa thati Njugush kuwa gari hilo la kifahari ni bora zaidi kuliko gari la Njugush.

"Timothy Kimani Ndegwa usiongee na mimi. Ukitaka kuzungumza na mimi andika barua pepe na nitakujibu ndani ya siku tatu hadi tano za kazi. Kimani kwisha wewe," Abel alimtania Njugush.

Kabla ya video hiyo ya gari lake jipya kuibuka, awali Mutua alikuwa amechapisha kwenye mtandao na kutangaza kuwa analiaga gari lake la zamani la Mercedes Benz.

Baba huyo wa mtoto mmoja aliandika ujumbe wa huzuni ulioambatana na video ya gari hilo likiwa limepakiwa kwenye lori.

Alilishukuru gari hilo kwa kumbukumbu za thamani na kumtumikia kwa miaka mingi.

Alikuwa amelipa jina la utani gari hilo Miss GT (God’s time)

"Na baada ya miaka mitano ya kupendeza, ni wakati wa kukuaga. Hili lilikuwa mojawapo ya magari bora zaidi ambayo tumewahi kuwa nayo. Kwa kweli inahisi aina fulani ya njia, lakini, lakini ujue, Mabadiliko hayaepukiki. Naomba Miss GT apate mmiliki mzuri kwa maana anastahili. Mlisema stage ya Kiambu ilihama pale Park Road ama nirisk tu?" aliandika mwigizaji huyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved