Mrembo mmoja katika mtandao wa Twitter amezua gumzo baada ya kudai kwamba anatafuta mwanamume wa kumvunja moyo kwa mapenzi ili apunguze kula kwani katika siku za hivi karibuni amegundua anakula sana.
Doyinsola David ambaye aliwahi kushiriki katika kipindi cha BBNija nchini Nigeria alikiri kwamba anatafuta mpenzi ambaye kigezo kikuu ni kuhakikisha atamvunja moyo katikati ya mahusiano yao.
Mshiriki huyo wa kipindi cha mazungumzo alilaumu ulaji wake wa kupita kiasi na kudai kwamba alitamani mpenzi angeuvunja moyo wake ili aanze tena kufanya kufuatilia kwa umakini ulaji wake, kwa kimombo ‘dieting’.
Kwa kuzingatia kiwango ambacho amekuwa mzito hivi majuzi, makisio yetu kutoka kwa makala yake yalikuwa kwamba kupokea dhiki ya kihisia kutoka kwa mpenzi wake wa kiume kungefanya kazi kama hirizi katika kumsaidia kupunguza uzito.
Aliandika; "Mtu kwa kweli anahitaji kuuvunja moyo wangu tena ... ili niende kwenye lishe. Kwa kweli naanza kula sana.”
Wengi haswa kina dada walifurika kwenye chapisho hilo la Twitter wakitoa maoni na ushuhuda wao jinsi walipunguza kilo za uzito wa miili yao baada ya kutendwa na waliokuwa wanawapenda.
“Namaanisha katika hali hiyo, huwezi kumaliza hata kipande kimoja cha mkate. Ni kama unakula nzima,” mmoja alisema.
“Safari hii hatutakuvunja moyo tu bali tutausambaratisha kabisa,” mwanaume alimtania.
“Usiwahi tamani kuvunjwa moyo haswa na mtu ambaye unampenda, dadangu utapoteza kilo hadi watu wa karibu na wewe wafikirie umeambulia virusi hatari vya UKIMWI, usitamani,” mwingine alimshauri.
Ni kweli kwamba kupitia masaibu ya kimapenzi humfanya mtu kupunguza kilo za uzito wa mwili?