logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Serikali ya 'wachamungu' yakosolewa kukubali Kinuthia kuingia ikulu na vazi la kike

Njohi alisema kuwa kuna wabunifu wa maudhui wenye ni wanyoofu ambao wangealikwa.

image
na Davis Ojiambo

Burudani10 June 2023 - 09:39

Muhtasari


  • • “Tuna waundaji wa maudhui wanyoofu kama vile mvulana anayeiga Riggy G, ambaye anaweza kuwa msukumo wa kweli kwa mvulana." - Njohi alisema.
Kinuthi akiwa kwenye ikulu kwa uzinduzi wa Talanta Hela.

Ijumaa kulikuwa na uzinduzi rasmi wa mradi wa Talanta Hela katika ikulu ya Nairobi ambapo waziri wa michezo na maswala ya vijana Ababu Namwamba aliwaalika wanablogu na wakuza maudhui ainati kuhudhuria mradi huo.

Mradi wa Talanta Hela unalenga kuwanufaisha vijana na haswa wale wenye talanta mbalimbali kutoka uigizaji, Sanaa, uimbaji na michezo kupata hela kutokana na vipaji vyao.

Hata hivyo, si wanablogu au wakuza maudhui wote walioalikwa au kuhudhuria na wengine ambao walihudhuria wamezua mjadala mkali mitandaoni.

Kwa mfano, sehemu ya watu mitandaoni walihoji kwa nini serikali ambayo imekuwa ikisema ina maadili ya kiafirika na kidini, mbona walimualika mwanablogu Kelvin Kinuthia ambaye skits zake huwa anazifanya akiwa amevalia mavazi ya kike hali ya kuwa yeye ni mwanaume.

Kinuthia aliwasili ikulu akiwa amevalia kawaida kama mwanamke katika vazi la rangi nyekundu na hilo lilionekana kugawanya wengi.

Mwanablogu maarufu katika mtandao wa Facebook, Council Njohi alikashifu hatua ya serikali kumwalika Kinuthia hali ya kuwa jinsi ya uvaaji wake haina kiashiria chochote cha heshima kwa mila na tamaduni za kiafrika na kuwaacha nje baadhi ya wakuza maudhui ambao skits zao ni za kimaadii.

“Tuna waundaji wa maudhui wanyoofu kama vile mvulana anayeiga Riggy G, ambaye anaweza kuwa msukumo wa kweli kwa mvulana. Hata hivyo kumweka Kinuthia kama kielelezo cha ubunifu na kumwalika Ikulu akiwa amevalia kama mwanamke ni kinyume na roho ya "Sisi ni Waafrika na Afrika ni Biashara Yetu." ... Hatupaswi kamwe kuacha matarajio yetu ya kitamaduni,” Njohi alisema.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved