logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize atangaza collabo na rapa wa USA, Mashabiki wahoji iwapo atamudu Kiingereza

“Kondeboy X Bobby Shmurda, napenda hii sauti bwana,” Harmonize aliandika huku akiweka emoji ya CD.

image
na Davis Ojiambo

Burudani29 June 2023 - 08:30

Muhtasari


  • • Katika moja ya picha hizo za screen, Harmonize alionekana akimtumia Shmurda mfululizo wa baadhi ya ngoma zake ikiwemo moja ambayo alikuwa amipa jina ‘Sef Made’
  • • Kutokana na maongezi hayo, Shmurda alionekana kuikubali ngoma hiyo na kumjibu Harmonize, “Kwa hakika Zaidi nataka tufanye hii.”
Harmonize atangaza collabo na rapa wa USA, Bobby Shmurda.

Msanii wa kizazi kipya kutoka Tanzania Harmonize amefanikiwa kupata shavu la rapa wa Marekani Bobby Shmurda akiwa katika ziara yake ya muziki nchini Marekani, ikiwa ni wiki kadhaa sasa.

Msanii huyo kupitia Instastory yake alifichua habari hizo akisema kuwa tayari wamefanikiwa kuingia studioni na Shmurda na kuachia kibao kimoja ambacho hata hivyo hakukitaja jina wala kuwapa mashabiki konjo chake, ila tu aliwahakikishia kwamba ni kibao kizuri.

“Kondeboy X Bobby Shmurda, napenda hii sauti bwana,” Harmonize aliandika huku akiweka emoji ya CD.

Itakumbukwa juma moja lililopita Harmonize alikiwasha mitandaoni baada ya kupakia picha za skrini akifichua maongezi yake na msanii huyo wa Marekani ambapo gumzo kubwa lilikuwa ni wao kutimba studioni na kujaribu kufanya collabo.

Katika moja ya picha hizo za screen, Harmonize alionekana akimtumia Shmurda mfululizo wa baadhi ya ngoma zake ikiwemo moja ambayo alikuwa amipa jina ‘Sef Made’ ambayo ni kama alikuwa anatarajia kuwashirikisha Sauti Sol.

Kutokana na maongezi hayo, Shmurda alionekana kuikubali ngoma hiyo na kumjibu Harmonize, “Kwa hakika Zaidi nataka tufanye hii.”

Hata hivyo, huku wengine wakimpongeza msanii huyo kwa kufanikisha kuipata sauti ya msanii mkubwa wa Marekani kwenye wimbo wake, wenye roho za korosha walionekana kumtupia dongo wakihoji iwapo atamudu kasi ya Kiingereza ‘cha kooni’ ambacho wengi wa wasanii wa Marekani wanaimba.

“Kaka hapo umejitia kitanzi, nasubiri kuona jinsi utakimbizana na kizungu cha mwamba huyo, mmoja alisema.

“Kimombo unacho?” mwingine alimuuliza.

Lakini haipiti bila kusemwa kwamab msanii huyo amejitahidi sana katika nyimbo zake za Kiingereza, huku goma la ‘Single Again’ likiwa linaendelea kukwea kwenye ngazi katika majukwaa mbalimbali ya kupakua miziki ndani ya nje ya Afrika.

Hivi majuzi pia Harmonize ameachia kibao kingine ‘Morning Call’ ambacho vile vile kinafanya vizuri.

Ikumbukwe miezi kadhaa iliyopita, Harmonize alijitangaza kuwa mfalme wa Bongo Flava na kudokeza nia yake ya kuacha kuimba nyimbo kwa Kiswahili ili kuingia katika soko la kimataifa kumenyana na wasanii wakubwa kwa lugha ya Kimombo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved