logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Aliyemburuza Davido mitandaoni kuavya mimba yake alia na kumuomba msamaha

Mrembo huyo aliwataka wanigeria kumsamehe kwa kuburuza msanii wao pendwa.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 July 2023 - 12:59

Muhtasari


  • • Chisom awali alikwa amejitokeza akidai kwamba aliwahi kuwa na mimba ya msanii huyo na hata kusema alimpa milioni 10 za Nigeria kuavya.
Mrembo aliyemburuza Davido aomba msamaha

Mrembo mmoja wa Nigeria kwa jina Chisom Flower ameomba msamaha hadharani baada ya awali kumkaripia msanii wa Afrobeats Davido akidai kwamba naye alikuwa na mimba yake.

Awali, mrembo huyo alifoka vikali kwenye mitandao ya kijamii akisema kuwa Davido aliwahi kumpa mimba ya hata kumpa Naira za Kinigeria milioni 10 ili kuavya mimba hiyo.

Mrembo huyo alikwenda hatua Zaidi kwa kupakia video ya mtu aliyedhaniwa kuwa Davido akiwa kwenye kitanda chake pamoja pia na ushahidi mwengine ulionuia kutia malalamishi yake nguvu na kuwaaminisha watu.

Mrembo huyo hata hivyo ameonekana kubadili msimamo wake baada ya kurudi kwenye mitandao ya kijamii na kumtaka Davido kumsamehe lakini pia akawaomba Wanigeria wote msamaha kwa kile alisema ni kutaka kumharibia msanii wao pendwa jina.

Alisema kwamab ameshapoteza kazi yak kutokana na tuhuma hizo na kumtaka ampe msamaha.

“Nimepoteza kazi yangu, familia na marafiki, hata chapa ninayofanyia kazi… Ninaomba radhi kwa David kwa kumkaripia hivyo na pia Wanigeria kwa kuvuta kipenzi chenu, naomba radhi.” Aliandika kwenye Instastory yake.

Chisom alijitokeza kusimulia kisa chake wakati Davido akiburuzwa mtandaoni na anayedaiwa kuwa ni mchepuko wake wa Marekani, Anita Brown na mchepuko wa pembeni wa Ufaransa, Ivanna, ambao wote walidai kuwa na ujauzito wake.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved