Msanii Wahu amewachekesha na kuwafurahisha mashabiki na wafuasi wake mitandaoni baada ya kufichua picha za zamani za mumewe Nameless jinsi alivyokuwa akionekana kipindi cha nyuma kabla ya umaarufu na pesa.
Nameless anatimiza mwaka mwingine Agosti 10 na kupitia ukurasa wake, mkewe Wahu alimsherehekea kwa kumuandikia ujumbe mtamu huku akiwapa nafasi mashabiki wao kujiunga katika safari ya msanii huyo mkongwe kwa kupakia picha za tangu akiwa mdogo, wakati anahangaika kutafuta maisha na baada ya kupata umaarufu na pesa.
Wahu alisema kwamba siku hizi mumewe hata hataki maneno mengi kwa kile alisema kuwa ni uzee kama umeanza kuwanyemelea.
“SIKU YA KUZALIWA YA BABA WASICHANA!!! πππππΎππΎππΎππΏππΏππΏππΏ Nimefurahi sana kusherehekea siku hii na wewe…hasa juu hautaki hadithi nyingi ππ(uzee manenos ππ) Kwa kweli ingawa ninamshukuru sana Mungu kwa ajili yako! Wewe ni kiongozi wa ajabu, baba na mwenzi wa maisha na wasichana na mimi tumebarikiwa kuwa na wewe. Happy birthday Bubu wangu!! Nyota yako iangaze daima usipungukiwe na Mungu aendelee kukupa nguvu na hekima katika maisha yako yote,” Wahu aliandika ujumbe.
“Life is a journey, enyewe watu hutoka mbali kama huyo ni Nameless alikuwa anakaa mtu wa mji” mmoja aliandika.
“Watu hutoka mbali, uzidi kung’ara,” mwingine alisema.
Anapofikisha umri wa miaka 47, baba wa wasichana watatu warembo anashukuru kwa furaha rahisi ambayo maisha yamemletea kwa miaka mingi. Katika taarifa yake ya siku ya kuzaliwa, alizidi kuwashukuru mashabiki wake kwa upendo ambao wameendelea kumuonyesha.
“BIRTHDAYBOY! π₯π₯π₯π₯ Nimebarikiwa na ninashukuru kwa furaha rahisi ambayo maisha yameniletea kwa miaka yote. Nawashukuru nyote kwa upendo mnaoendelea kunionyesha ninapofikisha mwaka mmoja!” aliandika.