"Wanasema nina watoto warembo" Mulamwah alalamika wanawake kumlilia awatunge mimba, awauzie mbegu zake

Mulamwah amefichua kuwa amepokea maombi mengi kutoka kwa wanawake wanaotaka kuzaa naye.

Muhtasari

•Mulamwah alifichua kuwa wanawake wengi wamemtumia jumbe wakiomba awatunge mimba tu na kuahidi kuondoka bila kudai chochote.

•Wakati huohuo, alisema hana uhakika kama rafiki yake wa karibu Ruth K ni mjamzito kama ambavyo Wakenya wamekuwa wakikisia.

Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Mchekeshaji na mtangazaji wa Kenya David Oyando almaarufu Mulamwah amefichua kuwa amepokea maombi mengi kutoka kwa wanawake wanaotaka kuzaa naye.

Katika mahojiano ya hivi majuzi na wanahabari, alifichua kuwa wanawake wengi wamemtumia jumbe wakiomba awatunge mimba tu na kuahidi kuondoka bila kudai chochote.

Baba huyo wa binti mmoja alidai kuwa baadhi ya wanawake hata wamejitolea kununua mbegu zake wakidai kwamba anazalisha watoto wazuri.

“Mimi niko busy sana. Hata huwa sioni mambo kuhusu wanawake. Wamejaa DM, wengine wanataka watoto na Mulamwah wanasema kwamba Mulamwah ako na watoto warembo, anasema anataka mtoto tu aende. Lakini sizingatii hilo,” Mulamah alisema.

Aliongeza, “Wengine hata wanataka kununua mbegu za kiume, wanasema Mulamwah niuzie na mimi nashangaa hizi ni gani.

Mchekeshaji huyo alisema hata hivyo amekuwa akikataa maombi yote. Pia aliweka wazi kuwa kwa sasa yupo sokoni kwani hayuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote.

Alipoulizwa kuhusu sifa anazotafuta kwa mwanamke wa kuchumbiana naye, aliweka wazi kwamba anataka mwanamke mwenye hekima kubwa.

“Saa hizi ni akili kwanza, mazee kuna watu warembo huku nje na akili hakuna. Mimi saa hii naangazia akili; unafikiria nini, unajiona wapi?, unataka kutimiza nini kama mwanamke? Heshima yako umeiweka wapi? Hizo ndizo nitaanza kupima kwanza kabla nikuje kwa muanekano wa mwili. Muonekano wa mwili mshaona watu nakaa nao kwa hivyo mnajua,” alisema.

Wakati huohuo, alisema hana uhakika kama rafiki yake wa karibu Ruth K ni mjamzito kama ambavyo Wakenya wamekuwa wakikisia.

Baba huyo wa binti mmoja alifichua kwamba bado hajapata dokezo lolote kwamba Ruth anatarajia mtoto wake wa kwanza.

“Mimi sijui, mimi sijui, mimi siwezi kutarajia mtoto, ningekuwa nimesikia akigonga kwa tumbo. Lakini nitamuuliza,” Mulamwah alisema.

Aidha, alishikilia kuwa mrembo huyo ambaye amekuwa akiigiza naye video za burudani ni rafiki yake tu na hakuna uhusiano wa kimapenzi kati yao.

Kuhusu tetesi za kumtunga mimba, alisema kuwa huenda mlimbwende huyo  na mpenzi wake wameamua kupata mtoto.

“Sijajua. Mimi nitamuuliza. Labda wameamua na mpenzi wake, sijui,” alisema.

Aliongeza, “Mimi huwaambia ako na chali yake kwa hivyo maisha yake siwezi kuingilia, labda mimi niulize kama nyinyi, jambo ambalo sio sahihi kwangu kufanya. Kama ni kitu atataka tujue basi bila shaka atatuambia.