logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hisia mseto Stevo Simple Boy akimpa shabiki wake zawadi ya shilingi 100

“Tutakuja baadaye alafu tukununulie ka lunch. Uko hapa karibu?"

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 September 2023 - 04:58

Muhtasari


  • • “Mimi na Khaligraph Jones ndio marapa wakubwa hii Kenya,” Stivo Simple Boy alinukuu video hiyo.
Stevo Simple Boy

Stivo Simple Boy, msanii wa kurekodi nyimbo za injili aina ya rap humu nchini, amewaacha mashabiki na watumizi wa mitandao ya kijamii katika hali ya mtanziko baada ya video kuibuka ikimuonesha akimpa shabiki wake zawadi ya takrima ya shilingi 100.

Video hiyo iliyozuka TikTok inamuonesha Stevo akiwa katika mizunguko yake ambapo alikutana na shabiki wake mmoja na kumuuliza ni wimbo upi ambao anaupenda kutoka kwa mfalme huyo wa misemo na nahau za kuvunja mbavu.

Baada ya kusalimiana, shabiki huyo alimtajia kwa furaha kwamba anaupenda wimbo wake wa Freshi Barida.

Stevo hakuchelewa Zaidi ya kuzama mfukoni na kutoa noti la shilingi 100 za kenya na kumpa shabiki huyo huku akimuahudi makuu baadae kama vile kumshughulikia utaalamu wa tumboni.

“Unapenda ngoma yangu gani?” Stevo Simple Boy aliuliza. Na kijana anajibu haraka na "Freshi Barida,"

“Tutakuja baadaye alafu tukununulie ka lunch. Uko hapa karibu? Stevo anaweza kusikika akimuuliza kijana, ambaye anajibu kwamba atasubiri wawili hao warudi.

Msanii huyo alifurahishwa na kumpongeza kijana huyo huku wawili hao wakiendelea kuongea bila kusikika kwa muda mfupi kabla ya Stivo, akiwa ameshika simu yake kwa mkono mmoja, kuchomoa noti ya Sh 100 na kumkabidhi kijana huyo.

“Mimi na Khaligraph Jones ndio marapa wakubwa hii Kenya,” Stivo Simple Boy alinukuu video hiyo.

Kujibu video hiyo, watumiaji wa mtandao wamechanwa. Wengine walifikiri kuwa pesa hizo ni ndogo sana na zilipakana na ukorofi, huku wengine wakimtaka Stevo asijaribu sana kupatana nao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved