Msanii namba moja kwa muda wote katika muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva kutoka Tanzania ambaye pia ni mjasiriamali, Diamond Platnumz amefichua kwamba katika maisha yake yote amefanya vingi lakini suala la kuvuta bangi hajawahi kufanya udhubutu hata siku moja.
Katika kipindi cha kujibu maswali na wanahabari wa Wasafi Media, Diamond na Zuchu waliwekwa kwenye kiti moto ambapo kila mmoja alikuwa anatakiwa kuchukua kijikaratasi kilichokuwa kimeandikwa swali na kukunjwa na kurushwa kwenye boksi.
Diamond alitoa kijikaratasi ambacho kilikuwa na swali lililolenga kubaini kama amewahi jihusisha na uvutaji wa bangi au dawa zozote za kulevya, jambo ambalo alilikanusha.
Hata hivyo, msanii huyo alisema kwamba kwa mara nyingi tu amejikuta katika hali ambayo ingemlazimu kuvuta bangi lakini amekuwa akikwepa mtego huo mara kwa mara.
“Dah kwa bahati mbaya mimi mitaani kulikuwepo kuna bangi nyingi zimeshawahi kunipitia kushoto, sikumbuki... kiukweli hapana sijawahi vuta bangi,” Diamond alisema huku Zuchu akimsisitizia kuona kama kweli atabadili jibu lake.
Awali tuliripoti kwamba msanii huyo alikiri kwamba hajawahi toka kimapenzi na mwanamke mwingine Zaidi ya Zuchu, licha ya kujulikana kuwa ni baba kwa watoto wanne na kina mama tofauti.
Katika swali hilo la awali, Zuchu pia aliwashangaza wengi alipofichua kwamba Diamond ndiye mwanamume wake wa kwanza kulala naye kimapenzi na kumpa usichana wake.
Wawili hao kwa Zaidi ya mwaka mmoja sasa wamekuwa wakiotesha uwezekano wao wa kuwa wapenzi licha ya kwamba pia uhusiano unaojulikana Zaidi ni wa kikazi ule wa mwajiri na mwajiriwa wake katika lebo ya muziki wa Wasafi.