logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hatua kubwa! Cardi B amtambua TikToker wa Kenya

Msanii marufu kumtambua mkenya tiktoker @lilroxanne.

image
na Davis Ojiambo

Burudani14 September 2023 - 10:44

Muhtasari


  • •Rapper huyo wa marekani alitoa maoni kuhusu video hiyo kwa kutuma emoji ya mapenzi
  • •lilipelekea Tiktoker huyo kushindwa kuzuia furaha yake na hivyo kuiweka wazi kwa mashabiki wake 

TikToker  wa Kenya afurahishwa baada ya mwanamziki maarufu rapper Cardi B kutoa maoni kwa video yake aliyochapisha wenye kurasa wake wa tiktok akipiga densi kwa muziki wa rapper huyo.

Hili lilipelekea Tiktoker huyo kushindwa kuzuia furaha yake na hivyo kuiweka wazi kwa mashabiki wake wanomfuatilia katika kurasa hiyo aisema;

"Mimi ni maarufu."

Si jambo la kawaida kwa wanamziki maarufu na wenye hulka kama ya Cardi B kuangalia video za watu ambao si wa hulka yake na kutoa maoni na hisia zao.

Rapper huyo aliyeshinda tuzo ya Grammy, alimtambua mkenya huyo anayetambulika kama @lilroxanne_ katika ukurasa wake wa tiktok baada ya kusambaa mtanadoni akipiga densi za kicheshi ambazo zinaendana sawia na muziki wa rapper huyo.

wimo huo wa bongo fleva  ulivuma mitandaoni kwa kasi na kushabikiwa kwa nambari kubwa zaidi ya mashabiki wa wapenzi wa nyimbo za bongo.

@lilroxanne alicheza kwa bidii wimbo huo maarufu na miondoko yake iliyosawazishwa kikamilifu  kupelekea kuvutia umakini wa Cardi B.

Rapper huyo wa marekani alitoa maoni kuhusu video hiyo kwa kutuma emoji ya mapenzi na kumuacha tiktoker huyo akiwa na furaha yenye kumbukumbu ya daima.

Alishiriki skrini ya nyota huyo alivyoonyesha upendo wake kwake kwa kumtambua. Hili litchangi pakuwa katika ukuaji wa mwanadada huyo kwa mitandao ya jamii.

Kwa kuzingatia kuwa ulimwengu wa sasa unasonga kwa kasi kiteknolojia na kwamba watu wengi hasa vijana wanajishirikisha kuonyesha talanta zao mitandaoni.

Hili linaashiria wazi kuwa ni vyema wasanii waliobobea kwa kiasi kikubwa kuonysha kujali na kuwatambua wale ambao ni chipukizi kama njia mojawapo ya uwashika mkono wa kuwainua ili nao watambulike.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved