Mwigizaji Carrol Sonie amevunja kimya kuhusu uhusiano uliopo baina yake na baba wa mtoto wake Mulamwah, miaka miwili baada ya kutengana kimapenzi.
Akizungumza na Nicholas Kioko, Sonie alikiri waziwazi kwamba bado ana namba ya Mulamwah kwa simu yake wala hakuifuta licha ya mchekeshaji huyo kutoa matamshi hasi dhidi ya Sonie na binti yao baada ya kuachana.
Sonie alikuwa anajibu chapisho ambalo aliweka Julai akisema kwamba kijibaridi kikali kilikuwa kinamweka kwenye majaribu ya kumpigia simu Ex wake.
Akiulizwa kama ni Mulamwah alikuwa anataka kumpigia, Sonie alisema kwamba si yeye kwani maEx wengine wapo lakini tu watu waliamua kuchagua kufikiria kwamba ni Mulamwah kwa sababu ndiye walikuwa wanajua.
Hata hivyo, alisema kwamba namba ya Mulamwah ako nayo lakini akadinda kuweka wazi iwapo mawasiliano baina yao bado yanaendelea.
“Sikuwa najaribu kumshambulia mtu, nafikiri watu wako na dhana nyingi tu kwa sababu wanamjua Ex mmoja sasa kila kitu kitakuwa kinazunguka tu kwa huyo Ex. Si kabla ya huyo mtu [Mulamwah] kulikuwa na maisha hata baadae. Mimi sikuwa namlenga Mulamwah, kama ni yeye nilikuwa nalenga si niko na namba yake, si ningempigia tu. Namba yake ninayo, kwa nini nisikuwe nayo sasa,” Sonie alisema huku akikataa kabisa kuendelea kufunguka iwapo wanaongea.
Akiulizwa iwapo aliona chapisho la rafiki wa Mulamwah ambaye anatajwa kuwa mpenzi wake mpya, Ruth K, aliyechapisha kama kumjibu Sonie kuhusu mawazo wa kumpigia Ex [Mulamwah] simu, Sonie, alisema kwamba hata hamjui.
“Mimi sikujua, siku hizi kusema ukweli hata wewe ndio umeniambia. Sikuwa najua. Mimi kuniona mitandaoni ni ngumu sana nina mambo mengi. Lakini sijui kabisa na wala huyo Ruth K mimi simjui, sijawahi muona,” Sonie alisema.
Sonie pia aliweka wazi kwamba Mulamwah hakushughulika katika kusherehekea binti yao Keilah siku yake ya kuzaliwa, akisema kwamba alikuwa tu yeye na mwanawe.