logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Andrew Kibe awashauri wavulana dhidi ya kuchumbiana na warembo walevi

Ameshauri kuwa wanadada wengi wanatumia hii mbinu kuwaweka waume wengi kwenye mitego

image
na Davis Ojiambo

Burudani22 September 2023 - 14:39

Muhtasari


  • • Ameeleza kuwa tabia za wanadada kulewa ni za kisasa kwani hazikuwahi kushuhudiwa tangu hapo awali akisema wanadada wa awali walikua wanajiheshimu wao pamoja na watu wa jamii.
Andrew Kibe/Instagram

Muunda maudhui maarufu Andrew Kibe, amewashawishi vijana wa kiume waepuke kuchumbiana na wanadada ambao wanabugia pombe kali.

Kibe amesema kwamba kuchumbia mwanadada mlevi ni kujiletea aibu kwa familia na kwa jamii kwa jumla, kutokana na tabia ya aibu wanayoonyesha pindi tu wakilewa.

Ameeleza kuwa tabia za wanadada kulewa ni za kisasa kwani hazikuwahi kushuhudiwa tangu hapo awali akisema wanadada wa awali walikua wanjiheshimu wao pamoja na watu wa jamii.

Hata hivyo Kibe amewashauri vijana, hasa wa kiume kuwa, ikiwa basi itatokea wamelewa kwa pombe wakiwa pamoja,wasijaribu kuenda na wao nyumbani kwao,ila ni afathali ujulishe watu wa familia yake wakamchukue nyumbani.

"Afadhali uite watu wao waje wamchukue kutoka mahali mlipo,kwa sababu ikiwa mtaenda naye, kisha ajipate asubuhi ifuatayo akiwa kwako , aibu itamshika na huenda akaanza kuongea mambo ya aibu,jambo ambalo litawapelekea kijana wa kiume kutiwa mbaroni."

Ameshauri kuwa wanadada wengi wanatumia hii mbinu kuwaweka waume wengi kwenye mitego ambayo huwarudisha nyuma kimaendeleo.

Kwenye kanda ya video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa TikTok , Kibe ameonya vijana wa kiume kuwa makini na mienendo yao ya maisha ili kuepuka kujisababishia lawama na kujitwika majukumu yasiyo na msingi.

Mashabiki wake walionekana kufurahikia ushawishi huo,huku wakimshukuru na kusema kuwa wamejifunza mengi kutokana na ushauri huo.

Abrah Shepherd mtumiaji wa mtandao huo alimjibu Kibe akisema;

"Asante sana Kifee,nimejifunza mengi kutoka kwa ushahuri huu."

Ni ushauri ambao unachukuliwa kama njia moja ya kuelimisha jamii hasa vijana wa kisasi cha sasa kujifunza na kujua mambo ambayo ni ya kujenga uhusiano kati ya vijana na jamii kwa jumla.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved