logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond adondokwa na chozi zito jukwaani akimlilia Zuchu, "Je utanipenda?"

Kwenye tamasha hilo la Sumbawanga, Diamond kwa mara nyingine tena alitia fora kwa ubunifu wa aina yake.

image
na Davis Ojiambo

Burudani25 September 2023 - 09:32

Muhtasari


  • • Msanii huyo alijiongeza kwa ufundi na kuliondoa jina la aliyekuwa mpenzi wake kipindi hicho – Zari – ambaye alimtaja kwenye wimbo asili na wakati vwa kutumbuiza aliweka jina la Zuchu.
Diamond Platnumz.

Msanii Diamond Platnumz amepekea huba lake na msanii wake Zuchu katika kiwango kingine baada ya kumlilia kumpenda hadharani mbele ya umati kwenye jukwaa.

Diamond alikuwa anatumbuiza kwenye mwendelezo wa tamasha la Wasafi, awamu ya mkoa wa Sumbawanga ambapo aliwarudisha mashabiki nyuma miaka 8 nyuma kwa kuwatumbuizia kibao cha 2015 – Utanipenda.

Hap ndipo mzuka ulipanda na Diamond kupiga goti kwenye jukwaa akiimba kiitikio na kuliingiza jina la Zuchu akimuuliza maswali kama atampenda kesho ikiwa mambo yake yatakwenda fyongo.

Msanii huyo alijiongeza kwa ufundi na kuliondoa jina la aliyekuwa mpenzi wake kipindi hicho – Zari – ambaye alimtaja kwenye wimbo asili na wakati vwa kutumbuiza aliweka jina la Zuchu.

“Bado nawaza sana, je itakapofika tama Zuchu utanipenda?... na magazeti yatanibwaga utasikia tafarani eti mpaka kwa Zuchu nimemwagwa na venye nilivyo mnyonge,” Diamond alimaliza kwa sauti ya kilio huku umati ukimshabikia.

Diamond waliachana na Zari mwaka 2018 baada ya kuwa pamoja kwa takribani miaka 5 na watoto wawili juu.

Tangu hapo, wote wamekuwa wakijihusisha na wapenzi tofauti tofauti, kila mmoja akijaribu kadri ya uwezo wake kupunja maisha.

Itazame video hii kuanzia dakika ya 9 na sekunde 14 kuona jinsi mapenzi ya Zuchu yanavyomtaabisha Diamond. 

Diamond kwa sasa amekuwa akidaiwa kuchumbiana na msanii chini ya lebo yake – Zuchu – licha ya kwamba uhusiano wao haujawahi kuonekana kuwa wa kweli, baadhi wanahisi wawili hao wanaigiza mapenzi ili kusukuma kazi zao za miziki.

Kwenye tamasha hilo la Sumbawanga, Diamond kwa mara nyingine tena alitia fora kwa ubunifu wa aina yake.

Safari hii alitokea kama mwanamieleka wa kutokea mataifa ya Uchina au Japan, akiwa amevalia mawanda ya kupigana mieleka kwa kimombo Martial Art.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved