Mkurugenzi wa lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide Harmonize ametangaza kwamba atakapompata mpenzi wake mpya, atafanya marudio ya kile alichomfanyia aliyekuwa mpenzi wake Kajala Masanja.
Harmonize kupitia Instagram Story yake, alipakia video akiwa kwenye gari lake na kuangaza kamera kwenye bango kubwa la kibiashara kando ya barabara ambapo aliandika kulipia bango kubwa la picha ya mpenzi wake mpya.
“Tunaonane hivi karibuni kuna picha ya mtoto mzuri itakuwa kwenye hili bango,” alisema kwenye klipu hiyo fupi.
Itakumbukwa mwaka jana alipokuwa akijaribu mbinu zote za kuliwinda penzi la Kajala, Harmonize alimfanyia mrembo huyo vitu vikubwa vya kustaajabisha ikiwemo kumnunulia zawadi ya gari aina ya Range Rover lakini pia kulipia picha yake kubwa kwenye bango hilo ambalo alionesha kwenye video hii.
Hili lilichangia pakubwa kwa Kajala kukubali kumrudia baada ya kuachana 2021 lakini penzi lao jipya halikuweza kudumu Zaidi ya miezi 6.
Jumatano, Harmonize kuputia ujumbe mrefu kwenye Instagram yake alisema kwamba kwa sasa hayuko kwenye mahusiano lakini akafichua kuwa kuna mwanadada amabye anamvizia na endapo atamkubali basi hivi karibuni atawajulisha mashabiki wake.
Baadhi ya mashabiki wanahisi kwamba msanii huyo analenga kutupa ndoana yake kwa mwanamitindo Hamisa Mobetto ambaye licha ya kuweka wazi kuwa yuko kwenye mahusiano na raia wa Togo, Harmonize ameonekana kumnyemelea na hata kumtungia wimbo wa Freestyle na pia kutumia picha yake kama DP yake.