logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu wengi hudhani mimi ni wazimu - Embarambamba

walinifanyia utafiti ili kudhibitisha akili yangu ni timamu Embarambamba asema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani26 October 2023 - 08:34

Muhtasari


  • •Embarambamba alizua minong’ono mitandaoni wiki chache zilizopita kwa kibao chake cha ‘Nataka Kunyonywa’ .
  • • Msanii  huyu kisha alirejea siku chache  na kibao kingine chenye utata kwa jina ‘Panua’.

Msanii wa injili mwenye utata kutokana na maudhui ya nyimbo zake, Embarambamba amefunguka na kusimulia jinsi ambavyo watu wengi hudhani yeye ni ana kichaa kwa jinsi ambavyo husakata densi kwenye video za muziki wake.

"Mfumo wa kucheza kwenye matope wakati wa mvua ni jambo la kawaida kwangu watu wengi hudhani nimerogwa huku wengine wakiniambia nimepoteza akili zangu ila kwangu jambo hili nalifanya ili kumtukuza Mungu kwa kumchezea densi", alisema .

Embarambamba alizua minong’ono mitandaoni wiki chache zilizopita kwa kibao chake cha ‘Nataka Kunyonywa’ msanii  huyu kisha alirejea siku chache  baadaye na kibao kingine chenye utata kwa jina ‘Panua’.

Msanii huyu amefichua kwamba kwa wakati mmoja madaktari wa kuchunguza afya ya akili walizuru nyumbani kwake kumfanyia ukakuguzi na kudhibitisha kwamba akili yake ni timamu.

Baada ya mahojiano  msanii huyu alidokeza kuwa Licha ya wengi kuhisi kwamba anaimba mambo ya kutukuza anasa akijificha ndani ya jina la utakatifu, alisema kwamba yeye anaimba injili ila wafuasi wengi ndio wanaomchukulia vibaya wakiwa na fikira za anasa.

Msanii huyu  alisimulia kuwa sehemu ya wimbo huo aliimba akimtaka Mungu kupanua  baraka kwa njia ambayo iliwaacha wengi wakidhani huenda anaimba mambo tofauti na injili.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved