Katika ulingo wa burudani, kuna nyakati ambapo waimbaji wakubwa hukusanyika ili kuunda bendi zinazofanya vizuri zaidi ya mawazo yao au matarajio ya jamii. Wanaishia kuunda muziki unaovutia hadhira kote ulimwenguni na kujulikana kwa nyimbo zao katika aina waliyochagua.
Hata hivyo, huku wakiwa na sifa zao, baadhi ya bendi za muziki hufanya uamuzi mkubwa wa kuachana, na kuacha kumbukumbu zisizofutika.
Baadhi ya bendi hubadilika kutoka ushirikiano mzuri hadi njia tofauti, huku wanachama wakiwa wanajishughulisha na kazi za peke yao au kufuata njia na tasnia tofauti kabisa.
Hiki ndicho kisa cha bendi ambazo, kwa muda, zilisimama kwenye ukingo wa ukuu kabla ya kufanya chaguo kuu la kuanza safari mpya, ndani na nje ya uwanja wa muziki.
Hizi hapa ni bendi zilizofanya uamuzi mgumu na kuacha kumbukumbu kubwa kwa mashabiki wao:
1.Sauti Sol- Kikundi hiki kilitengana baada ya miaka 18 ya kukonga nyoyo za Wakenya na hadhira za kimataifa wakiwemo marais, kikundi hiki kurudi nyuma kwa muda usiojulikana kutoka kwa miradi shirikishi kama bendi.
Hata hivyo, walifafanua kwamba hawakuwa wakiachana kama kikundi au biashara bali walihitaji wakati wa kujiliwaza kama watu binafsi wa muziki.
2.Kelptomaniax- Kuanzia Tuendelee, Haree, na Furahia hadi Magnetic na Psycho, kikundi hiki cha hip-hop kilitawala uimbaji wa muziki wa Kenya mwanzoni mwa miaka ya 2000. Nyashinski, Collo, na Robert walikuwa walikuwa wameungana lakini, maamuzi yalifanywa, na kundi kugawanyika. .
3.Tatu- Angela Mwandanda, Angie Ndambuki, na Debbie Asila walikuwa bendi ya it girl enzi zao. Walitoa club bangers na kushirikiana na majina ya juu katika eneo la muziki wa Kenya.
Walakini, kikundi kiliamua kugawanyika na kufuata kazi tofauti. Katika mahojiano ya awali, Bi Angela alisema mkutano ulikuwa mezani kila mara lakini ratiba na umbali kati ya wanabendi hao wa zamani ulifanya majadiliano kusitishwa kwa miaka mingi.
4.Camp Mulla- `The rich kids of Kenya`,ndivyo walivyojulikana waliungana kuachilia muziki ambao haukutarajiwa nchini Kenya. Kundi la Hip Hop lilitoa muziki sawa na ule Wamarekani ubora wao wa sauti na video ulikuwa wa hali ya juu.
Hata hivyo, katika kilele cha taaluma yao, kikundi kiligawanyika mnamo 2013. Bi Karun aliondoka nchini kwa elimu yake ya chuo kikuu huku mwanachama mwingine akichagua kazi ya peke yake. Hii iliashiria mwanzo wa mwisho wa bendi. Party Don’t Stop ilikuwa mojawapo ya nyimbo zao kubwa zaidi .
5.Neccessary Noise-bendi hii iliundwa na mwanamuziki Nazizi Hirji,Kevin wyre na rrapper Bamzigi.
Hila kilitendana mnamo mwaka wa 2006,kutokana na mzozo wa wanachma wa bendi.