logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pasta Ezekiel ataka wasanii kuchuguza tunzi zao akirejelea wimbo wa -Moji Short Baba

Moji Short Baba asema kuwa yeye huimba kumtukuza Mungu si mwanadamu.

image
na Davis Ojiambo

Burudani08 November 2023 - 07:49

Muhtasari


  • •Kuimba isiwe ni kwenda tu studio na kutoa ngoma ili kumfurahisha mwanadamu ila kuwe kwa utunzi wa nyimbo zenye mfano mwema na zenye misamiati ya heshima kwa Mungu alisema
Moji Shortbabaa na Pasta Ezekiel

Mchungaji wa kanisa la New life Prayer Center Mavueni Ezekiel Odero amewataka wasanii wa nyimbo za injili kuchunguza utunzi wa nyimbo zao ili ziwe zenye  maadili mema yanayotukuza jina la Mungu.

Kiongonzi huyo wa kanisa alisema hayo wakati wa ibada na wafuasi wake huku akiwaonesha kwa kutoa mfano wa video ya Wimbo wa msanii wa nyimbo za injili  almaarufu Moji Short Baba.

Wimbo wenye maneno "oyooyoo  ayayaaa densi ya kanisa densi ya kanisa," maneno kwenye wimbo yalisema.

"Mnataka kumtukuza Mungu kwa nyimbo kama hizi,hakuna mtu ako na ladha ya miziki kama hizi,hata sauti iwe  inasifiwa sana  hakuna anaye taka kumtukuza Muumba wake Kwa nyimbo hizi,"alisema mchungaji Ezekiel.

Mchungaji huyu aliendelea kutoa kauli yake kwa wafuasi wake akisema kuwa si kuimba tu kunamfuraisha Mungu ila ni yale maneno ya heshima kwa utunzi wa msanii kwa kumtukuza Mungu.

"Kuimba isiwe ni kwenda tu studio na kutoa ngoma ili kumfurahisha mwanadamu ila kuwe kwa utunzi wa nyimbo zenye mfano mwema na zenye misamiati ya heshima kwa Mungu alisema.

Baada ya msanii huyo kufanyiwa mahojiano ya moja kwa moja na mwanablogu kulingana naye wimbo wake ni wa kumtukuza Muumba wake ila si tu kufurahisha wanadamu.

"Mimi huimba kumtukuza kristo si kumfurahisha mwanadamu,"alisema msanii huyo wa Injili.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved