Taraja Ramsess, mwigizaji na msanii wa karate anayejulikana kwa kazi yake kwenye filamu za "Black Panther" na "Avengers", anaombolezwa baada ya yeye na watoto wake watatu kuuawa kutokana na ajali ya gari huko Georgia wiki iliyopita.
Alikuwa na umri wa miaka 41 tu.
Kituo cha Televisheni cha Atlanta WSB-TV kiliripoti kwamba ajali hiyo ilitokea kabla ya saa sita usiku siku ya Halloween baada ya gari Ramsess na watoto wake waliokuwa wakisafiria kugongana na trela ya trekta ambayo ilikuwa imeharibika katika njia ya kushoto ya njia ya kutoka nje ya barabara.
Mama yake, Akili Ramsess, mpiga picha ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Kitaifa cha Wapiga Picha wa Vyombo vya Habari nchini Marekani, alitangaza kifo chake na cha mabinti zake wawili katika chapisho la Instagram.
"Mwanangu mtanashati, mpendwa na mwenye talanta Taraja @chop.saki, pamoja na wajukuu zangu wawili, binti yake wa miaka 13 Sundari na binti yake mchanga Fujibo mwenye umri wa wiki 8, waliuawa usiku uliopita katika ajali mbaya ya barabarani," aliandika.
Pia aliandika kwamba mabinti wawili wa Ramsess walinusurika kwenye ajali hiyo, na mtoto wake wa miaka mitatu, Shazia, amelazwa hospitalini na mtoto wake wa kiume wa miaka 10, Kisasi, ambaye aliandika kwamba alikuwa kwenye chumba cha dharura.
Katika chapisho lililofuata, alishiriki kwamba Kisasi pia alikufa.
Ramsess anajulikana sana katika sifa zake za kuigiza katika filamu mbalimbali zikiwemo pamoja na “Avengers: End Game,” “Black Panther: Wakanda Forever” “Creed III,” “The Hunger Games: Catching Fire” na “She-Hulk: Attorney at Law.”