Seneta maalum Karen Nyamu na mpenzi wake, afisa wa polisi ambaye pia ni msanii wa Mugithi, Samidoh wanazidi kuonesha kila sababu ya upendo wao pasi na kujali kile ambacho wale wanaoegemea mrengo wa Edday Nderitu wanasema kuwahusu.
Wapenzi hao wawili walipeleka mapenzi yao katika kiwango kingine baada ya kuabiri bodaboda pamoja na kurekodi tukio hilo.
Katika video hiyo ambayo Nyamu aliipakia katika ukurasa wake wa Instragram, alikuwa ameketi nyuma tu ya mwendesha boda huku Samidoh akiwa kama nguzo nyuma kabisa.
Nyamu ndiye alikuwa anarekodi tukio hilo na kuonesha jinsi ambavyo Samidoh alikuwa amefurahi kuabiri naye bodaboda huku akishindwa kuzuia tabasamu, kwani wanasema utamu wa bodaboda ni kubanana.
“Tuma pin weekend ianze sasa, ata nimesha pandishwa nduthi ,” Nyamu aliandika.
Wafuasi wao katika mitandao ya kijamii walidakia katika chapisho hilo na kusema kwamba kwa muda mrefu Samidoh alikuwa amejificha katika penzi la Edday lakini kumbe alikuwa anatamani sana penzi kama la Karen Nyamu – penzi la kujaribu vitu vipya na kuonesha ulimwengu kama tukio hilo la kuabiri boda pamoja.
Haya hapa ni baadhi ya maoni kutoka kwa mashabiki;
“bluetooth imeunganishwa kwa mafanikio,” aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko aliandika.
“Si Bien amesema usipandishe dem nduthi ama… #MaCherie love to see it!” Mtangazaji Kwambox alisema.
“amidoh amesema mambo ya kutuma Fare inakuliwa na hii uchumi Nefa efa! Mwanaume ni kujituma,” Chris Kirwa.
“Hapa nikama nothing but prayers alikua anaforce” Msnabea alisema akimaanisha kauli ambayo hutumiwa sana na Edday Nderitu.
“Si mnajuwa kutoa meno nje mkiwa pamoja😂 mapenzi shikamooo” Wakesho wahida.