logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Alikiba awalipa mashabiki kwa picha ya selfie ili kuchanga pesa kwa wakfu wa Prof Jay

Msanii huyo alizunguka meza baada ya nyingine na kuchangisha pesa kwa ajili ya flash ile.

image
na Davis Ojiambo

Burudani11 December 2023 - 11:28

Muhtasari


  • • Alikiba katika hafla hiyo alipewa kibarua kimoja tu, kuuza flash yenye nyimbo ndani mwake kwa kiasi cha shilingi milioni 2 za kitanzania.
Alikiba na Professor Jay

Msanii Alikiba wikendi iliyopita alionesha mdano mzuri wa kuigwa baada ya kutokea kama mgeni wa heshimu katika hafla ya uzinduzi wa wakfu wa msanii mkongwe Professor Jay.

Professor Jay alikuwa anazindua wakfu wake kuchangisha pesa za kuwasaidia wenye shida za figo, tatizo ambalo lilimuathiri na kumfanya kuwa mgeni wa madaktari kwa Zaidi ya mwaka mmoja.

Alikiba katika hafla hiyo alipewa kibarua kimoja tu, kuuza flash yenye nyimbo ndani mwake kwa kiasi cha shilingi milioni 2 za kitanzania.

Msanii huyo kwa weledi mkubwa aliwaomba mashabiki wake kutomuangusha kwa kumsaidia kupata kiasi cha milioni mbili kwa hiyo flash.

Aliwaahidi mashabiki wake kuwa kila mmoja ambaye angekuwa radhi kuchangia katika mfuko wa wakfu huo basi angemlipa kwa kupiga naye picha ya selfie ya kukumbukwa.

“Mashabiki wangu, mashabiki wa wasanii wengine, mashabiki wa Alikiba naombeeni msiniangushe, hii flash natakiwa niuze haraka tutimize milioni mbili. Au mwenye milioni 2 aje moja kwa moja ili niweze kuwa nimemaliza hili zoezi. Mimi napiga selfie mtu akitoa hela, napiga naye selfie,” Alikiba alisema kabla ya kuchukua kikapu cha hela kuwafuata mashabiki wengi ambao walimnyooshea mikono tayari kuchangisha ili kupata picha naye.

Msanii huyo alizunguka meza baada ya nyingine na kuchangisha pesa kwa ajili ya flash ile.

Itakumbukwa Professor Jay alitarajiwa kuzindua wakfu wake Novemba 24 lakini kutokana na matukio mengi siku hiyo yakiwemo lile la Harmonize kuachia albamu yake, alilazimika kusongeza mbele.

Awali, wabunge nchini Tanzania walifanya michango katika majengo ya bunge kwa ajili ya wakfu huo, ikizingatiwa kwamba msanii huyo aliwahi kuwa mbunge kwa muhula mmoja kabla yak kubanduliwa katika uchaguzi wa 2020.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved