logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akothee alalamika marafiki kumtenga wakati alihitaji msaada kuendeleza shule yake

"Lakini kama ni pombe wangeninunulia champagne ya 17k"

image
na Davis Ojiambo

Burudani17 January 2024 - 08:16

Muhtasari


  • β€’ Mwishoni mwa mwaka jana, Akothee alizindua rasmi shule yake chini ya wakfu wake na kusema kwamba ilikuwa moja ya ndoto zake za muda mrefu zilizotimia.
Akothee

Msanii na mjasiriamali Akothee ameonesha kutofurahishwa kwake na watu ambao alikuwa anawachukulia kama marafiki zake wa karibu kumkwepa wakati aliwahitaji kwa msaada wa kufanya jambo la maana.

Akothee kupitia kurasa zake za mitandaoni alichapisha ujumbe mrefu akielezea safari ya kuistawisha shule yake ya Akothee Academy na kusema kwamba umekuwa wakati mgumu ambao amejikuta akiwa peke yake bula msaada.

Msanii huyo alisema kwamba marafiki zake walimkatia umeme wakati alihitaji msaada hata wa kununua dawati, akisema kwamba ingekuwa ni sherehe wengi wangemnunulia hata ile pombe ghali lakini kwa suala kama hilo la kuinua jamii, wote wamechimba mitini.

“Mwaka huu mikono yangu imejaa Akothee Academy. Hata marafiki niliodhani wangeniunga mkono nimekula ma blue ticks kibao πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nang’ang’a mwenyewe hata desk ya 3500 hawawezi ninunulia lakini kama ni pombe wangeninunulia champagne ya 17k πŸ™ tena wangeniuluza ni hoteli Gani nataka kwenda,” Akothee alisema.

Aliahidi kumsaidia kijana mmoja kujiunga katika shule ya upili, akisema kuwa picha ya huyo mvulana mdogo mwenye uhitaji mkubwa alikutana nao mitandaoni na kuomba kuelekezwa ili kumfikia.

“Lakini kwa huyu kijana naweza kuachana na 10k. Yeyote aliye na maelezo yake ya kututumia. Nimefika tu kwenye Facebook πŸ™ Kijana huyu anaomba watu wenye mapenzi mema kumsaidia kujiunga na Withaga Boys katika Kaunti ya Murang'a. Mvulana huyo kutoka Gatundu Kaskazini alipata alama 379 katika KCPE lakini familia yake haina uwezo wa kufadhili masomo yake ya upili. Baba huyo amenukuliwa akisema kuwa amejaribu kutafuta msaada bila mafanikio,” Akothee alisema.

Mwishoni mwa mwaka jana, Akothee alizindua rasmi shule yake chini ya wakfu wake na kusema kwamba ilikuwa moja ya ndoto zake za muda mrefu zilizotimia.

Akothee aliwahi nukuliwa akieleza jinsi alilazimika kusitisha safari yake ya kusomea digrii kwa hadi miaka 7 ili tu kuhakikisha anafanikisha ndoto ya kuwaelimisha watoto kwa elimu ya msingi ambayo alisema lengo lake ni kuwapa watoto maskini elimu ya kuwawezesha japo kujua kusoma na kuandika tu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved