Msanii Nandy baada ya kupost picha yake halisi ikionyesha muonekano wake bila chagizo, alipata baadhi ya watu haswa wanawake ambao walianza kumkejeli kwa jinsi tumbo lake lilivyokuwa likionekana na michirizi, kwa kimombo ‘stretch marks’.
Jambo hili lilionekana kutokaa sawa na Nandy na haswa kuona kwamba lilikuwa linatiwa moto na wanawake wenza, alihisi ni Zaidi ya usaliti na unyanyapaa.
Nandy aliamua kutoa maeleoz ya kina kuhusu picha hiyo na kusema kwamba aliaua kuipakia jinsi ilivyo kwa sababu anajikubali mwili wake na mabadiliko anayoyapitia baada ya kuzaa.
Nandy aliwasuta kina dada ambao hawataki kujikubali jinsi walivyo na kusema kwamba alikuwa na uwezo wote wa kuifanyia uhariri picha hiyo ili kuficha mapeto hayo lakini aliamua kuiachia jinsi ilivyo ili kuonesha uhalisia wake.
Msanii huyo anayezidi kutamba kwa kibao cha ‘Dah!’ akimshirikisha Alikiba alisema kwamba katu yeye hawezi kuficha chochote kwa lengo la kuwafurahisha watu kwani yeye ni mpambanaji wala si slay queen.
“Acha niwaambie jambo moja kina dada, mimi sio slay queen, mimi ni hustler, hiyo picha ningekuwa na kila sababu ya kuihariri msione chochote kwa sababu naweza. Nimeweka hivyo kwa sababu najivunia na kuonea fahari mwili wangu, na napenda nilivyo! Achene umbea na wivu, jikubalini mlivyo,” Nandy aliwafokea kina dada.
Nandy alisema kwamba baada ya kuzaa, michirizi kuna baadhi ya watu inawafanya kuwa wa kuvutia Zaidi na kwamba hilo ni jambo ambalo hutokea kwa takribani kila mama baada ya kuleta kiumbe kipya duniani, kwa hiyo haoni sababu ni kwa nini watu – haswa wanawake wenzake – kutumia fursa hiyo kumkejeli mitandaoni.
“Michirizi kuna baadhi ya wengine inawafanya kuwa sexy, na wengine inawafanya wanakaa vibaya. Zangu hizo 3 nazipenda jamani,” aliongeza.