logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtangazaji maarufu wa TV wa Marekani apatikana na tatizo la ubongo

Kipindi chake kiliisha mwaka wa 2022 huku kukiwa na shida za kiafya ambazo amekuwa akizikabili.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani23 February 2024 - 07:38

Muhtasari


  • •Bi Williams, 59, alikuwa mwenyeji wa kipindi cha Wendy Williams Show kilicho na umaarufu mkubwa kilichhokwenda hewani nchini Marekani kwa zaidi ya muongo mmoja.

Nguli wa kipindi cha mazungumzo cha mchana nchini Marekani, Wendy Williams Hunter, aligunduliwa mwaka jana kuwa na aphasia inayoendelea na matatizo ya ubongo ya frontotemporal (FTD), timu yake ya utunzaji imefichua.

Timu hiyo ilisema ilikuwa ikitoa habari hiyo "ili kurekebisha uvumi usio sahihi na wa kuumiza kuhusu afya yake".

Bi Williams, 59, alikuwa mwenyeji wa kipindi cha Wendy Williams Show kilicho na umaarufu mkubwa kilichhokwenda hhewani nchini Marekani kwa zaidi ya muongo mmoja.

Lakini kiliisha mnamo 2022 huku kukiwa na shida za kiafya ambazo amekuwa akizikabili.

Habari za kugunduliwa kwa matatizo hayo zinakuja siku moja baada ya jarida la People Magazine, ambapo jamaa walisema Bi Williams yuko katika kituo cha utunzaji katika eneo lisilojulikana na amekuwa katika hali ya kushangaza ya kiafya.

"Kama mashabiki wa Wendy wanavyofahamu, siku za nyuma amekuwa wazi kwa umma kuhusu mapambano yake ya kimatibabu na Ugonjwa wa Graves' na Lymphedema pamoja na changamoto zingine muhimu zinazohusiana na afya yake," timu yake ya utunzaji iliandika katika taarifa Alhamisi.

"Katika kipindi cha miaka michache iliyopita, maswali yaliibuka wakati fulani kuhusu uwezo wa Wendy wa kuchakata taarifa na wengi wamekuwa wakikisia kuhusu hali ya Wendy, hasa alipoanza kupoteza maneno, kufanya mambo yasio ya kawaidda wakati fulani, na kuwa na ugumu wa kuelewa miamala ya kifedha."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved