logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Embarambamba alilenga kufikia viziwi na wimbo ‘Niko Uchi’ – wakili Danstan Omari aiambia KFCB

Pia alilalamikia kiasi cha faini ambacho KFCB inamtaka Embarambamba kutoa.

image
na Davis Ojiambo

Burudani07 March 2024 - 08:32

Muhtasari


  • • Omari pia anasisitiza kwamba mteja wake ni mtumishi wa Mungu ambaye muda wote saa 24 kwa siku 7 za wiki anajitolea kumtumikia Mungu.
Omari na Embarambamba

Wakili wa msanii Embarambamba, Danstan Omari ameiandikia bodi ya KFCB barua ya kulalamikia matakwa na masharti makali ambayo walimpa msanii huyo kufuatia taharuki iliyotokea na wimbo wake mpya ‘Niko Uchi’.

Katika barua hiyo, Omari analalamika kwamba msanii huyo hakuwa analenga watu ambao wanalalamika kuhusu maudhui yake katika wimbo huo, bali lengo lake lilikuwa ni kuwafikia viziwi na ujumbe wake.

Omari pia anasisitiza kwamba mteja wake ni mtumishi wa Mungu ambaye muda wote saa 24 kwa siku 7 za wiki anajitolea kumtumikia Mungu na hivyo madai yanayoibuliwa kwamba maudhui yake ni ya kupotosha jamii si kweli.

“Mteja wangu ni mtumishi wa neno la Mungu na kazi zake za kibunifu siku zote amekuwa akizifanya kama kumtumikia Mungu na kuwavutia wengi kwa wokovu. Inashangaza kwamba badala ya kumpongeza mteja wangu kwa ubunifu alio nao, mumeamua kumkashifu na kumuua moyo kwa kumpa matakwa ya siyo sahihi,” sehemu ya barua hiyo iliyoonwa na radiojambo.co.ke ilisoma.

“Niko Uchi ni moja kati ya kazi zake za kibunifu ambazo zililenga kuwafikia viziwi ambao hawana uwezo wa kusikia ujumbe wake lakini bado wanaweza kuelewa ujumbe wake kutokana na kuona picha na video ya wimbo,” Omari aliongeza.

Wakili huyo maarufu pia alilalamikia kiasi cha faini ya milioni 6.4 ambazo KFCB inadaiwa kumtaka Embarambamba kulipa, akisema kwamba jambo hilo limemkosesha Amani kwani kama wanavyojua, Embarambamba kama wenzake hawajakuwa wakipokea mirahaba mizuri kutoka kwa bodi ya hakimili, MCSK.

“Mteja wetu, kama tu wasanii wengine nchini Kenya, anapokea mirahaba michache kutoka kwa MCSK, ukweli ambao pia nyinyi mnauelewa. Kutokana na hilo, mteja wetu ako katika hali ngumu ya kupata mamilioni ya fedha ambazo mlimtoza kama faini.”


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved