Muigizaji Terence Creative amefanya kufuru ya mwaka baada ya kufanya kitendo ambacho wengi hawakutarajia, na ambacho kimesifiwa kuwa suluhu kwa watu wenye husda mitandaoni.
Creative kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, amekuwa akifuatilia picha ambacho mkewe Milly Chebby anapakia na kuona jinsi baadhi ya watu wenye wivu wanavyomdhihaki kwa kusimanga maumbile yake.
Alichokifanya Terence Creative ni kuchukua picha za kila mmoja ambaye alikuwa anaandika maoni ya kumdhihaki Milly Chebby kutokana na umbile lake na kuzichapisha zote kwenye kurasa zake.
Terence alirundika picha hizo na kuweka wazi kwamba si za watu ambao wamepotea bali ni wale ambao wamekuwa wakimtukana mkewe mpendwa, lakini akasema kwamba ameshawasamehe.
“Hizi ndio baadhi ya picha za watu wanabody shame my beautiful wife Milly Chebby na kumpa fashion advice and beauty tips. Wow, nyinyi watu mko ni wa ajabu na tunawatakia mema katika nyakati hizi ngumu, tutatoboa pamoja,nimewasamehe na Mungu awabariki. Wakati huo huo wacha niendelee kusoma comments,” Terence alisema.
Hatua hii ilivutia maoni mseto, wengi wakionekana kumpa hongera Terence kwa kutumia njia isiyo ya vurugu kukomesha hulka ya watu ambao kazi yao mitandaoni ni kuona lisilo jema kwa maisha ya wengine.
Haya hapa ni baadhi ya maoni ya watu;
“Baadhi yao aki, heri tu wangejifunza kunyamaza,” Linnet Nafula.
“Sishangazwi na mwonekano wao. Usikune kichwa juu ya wapiganaji wa kibodi; maoni yao yanaonyesha kushindwa, hasira, uchungu, na upumbavu.” Mary William’s
“Watu wanaoumizwa huwaumiza watu .Usipoteze muda wako kwao. Wewe na Milly mnapaswa kuzingatia kutupa maudhui yanu mazuri.” Benter Oluoch