Msanii Jovial amewashauri wanawake kupata watoto tu wanapokuwa tayari, badala ya kutegemea mzazi wao wa jinsia ingine kusaidia.
Alishiriki maoni yake kwenye mtandao Instagram alipokuwa akijadili changamoto za kushirikiana katika malezi jambo ambalo limekuwa la kawaida.
"Kushirikiana katika malezi kumekuwa moja wapo ya shida zaidi duniani! Mara nyingi upande moja katika malezi huwa na uchungu, wakidhani wanelekeza machungu kwa wenzao wakati mwathiriwa halisi ni mtoto!” alisema.
Jovial alibainisha kuwa ingawa mabadiliko ya mwili yalizingatiwa kuwa jambo la kudhoofisha linapokuja suala la ujauzito, amegundua kuwa ni kipengele cha kiakili ambacho ni muhimu sana.
Unapowaambia watu wako wa karibu unapata mtoto wanakutishia na story za mwili ubadilika ujitayarishe kumbe unahitaji kujiandaa kiakili na kisaikolojia”
Aliwashauri wanawake badala yake wachague kupata mtoto wakati wao wenyewe wako tayari.
"Uwe na mtoto huyo wakati uko tayari kupata mtoto huyo!" Jovial aliongeza.