logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Butita kuandama na rais Ruto katika ziara ya USA kukutana na rais Joe Biden ikuluni White House

Ziara hiyo itang’oa nanga Alhamisi ya Mei 23 na rais Joe Biden anatarajiwa kuwa mwenyeji wao.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 May 2024 - 11:39

Muhtasari


  • • Ziara hiyo itang’oa nanga Alhamisi ya Mei 23 na rais Joe Biden anatarajiwa kuwa mwenyeji wa rais Ruto na kundi lake kutoka Kenya, katika ikulu ya White House.
Butita

Mchekeshaji aliyegeuka na kuwa mjasiriamali katika uzalishaji wa kidijitali, Eddie Butita amejawa na furaha baada ya rais William Ruto kumtaja miongoni mwa kundi la Wakenya atakaoandamana nao katika ziara rasmi ya mwaliko wa rais wa Marekani, Joe Biden.

Ziara hiyo itang’oa nanga Alhamisi ya Mei 23 na rais Joe Biden anatarajiwa kuwa mwenyeji wa rais Ruto na kundi lake kutoka Kenya, katika ikulu ya White House.

Akionyesha furaha yake, Eddie Butita kupitia ukurasa wake wa Instagram alichapisha picha akiwa amestarehe na kumshukuru rais Ruto kwa kumchagua kuwa miongoni mwa watu atakaoongozana nao katika ziara hiyo yenye haiba ya aina yake.

“Kuondoka kwenda Marekani leo. Asante Mheshimiwa Rais William Samoei Ruto kwa kunichagua kuandamana nawe katika Ziara ya Kiserikali ya Marekani iliyoandaliwa na Rais wa Marekani Mheshimiwa Rais Joe Biden,” Butita alisema.

Awali, iliripotiwa kwamba rais Ruto katika ziara yake ya Marekani, atazuru studio za uzalishaji muziki za Tyler Perry na washikadau wengine kadhaa katika mfumo wa ikolojia wa Hollywood ili kuwashirikisha jinsi wanavyoweza kufanya kazi na wbunifu wa Kenya.

Kwa nadharia hii, Butita ambaye ni mmoja wa wabunifu tajika katika kizazi cha sasa alisema kwamba atawakilisha washikadau wenzake katika tasnia hiyo vilivyo, akisema kuwa ni Dhahiri rais Ruto anajali maslahi ya wakuzaji maudhui.

“Ukweli kwamba mimi ni sehemu ya ujumbe wa Mkuu wa nchi ni ishara tosha na tunafurahi kwamba tasnia ya ubunifu ni sehemu ya mazungumzo ambayo tutakuwa nayo katika safari hii,” Butita alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved