Muunda maudhui wa Kenya, Commentator 254, ameelezea ubora wa kuchumbiana na mwanamke mwafrika.
Katika video iliyosambazwa kwenye mtandao wa Instagram, Commentator alisema kuwa baada ya siku nyingi kazini, huwa anatazamia kwenda nyumbani kwa mpenzi wake Moureen Ngigi kwa sababu ya mapenzi anayompa.
Wawili hao walishiriki video ya jinsi jioni yao hukuwa baada ya kufika nyumbani. Kwenye video Moureen anaonekana akimsalimia mlangoni, akichukua begi la ununuzi na kuvua koti lake. Kisha anaendelea kuchota beseni la maji ya joto ambalo anatumia kuosha miguu yake.
Moureen anaonekana akipiga magoti sakafuni huku akiosha miguu ya mtu wake na kuendelea kuikausha huku uso wake ukionyesha tabasamu na baadaye kumletea viburudisho.
Mashabiki hata hivyo wametoa maoni tofauti huku baadhi wakidai kuwa ni video iliyoandikwa inayolenga kutoa mwonekano.Huku wengine wakisema ishara ndogo kama hizo hufanya ndoa ifaulu.
Katika mahojiano ya awali na Nicholas Kioko, alifichua kuhusu kupatana na mpenzi wake, Moureen Ngigi, na jinsi alivyochukua nafasi yake.Commentator alisema kuwa Moureen ndiye aliyewasiliana naye baada ya kufikisha watu laki moja wanaofuatilia YouTube yake, na hapo ndipo mazungumzo yao yalipoanza. Wanandoa hao kwa sasa wako na mtoto mmoja kijana mwenye umri wa mwezi moja