logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kinuthia ashindwa kuzuia machozi baada ya mamake kumnunulia zawadi ya iPhone 15 pro max

Dada yangu na mama yangu walinishangaza kwa zawadi yangu ya ndoto - Kinuthia.

image
na Davis Ojiambo

Burudani22 May 2024 - 12:04

Muhtasari


  • • Baada ya kuichomoa, alipigwa na butwaa kupata ni simu aina ya iPhone 15 pro max yenye uwezo wa kubeba video na nyimbo kwa hadi 1TB.
Kelvin Kinuthia

Tiktoker Kelvin Kinuthia alishindwa kuzuia furaha yake baada ya wanafamilia wake kujumuika pamoja na kumfanyia bonge lla surprise.

TikToker huyo alichukua katika ukurasa wake wa Instagram kuonyesha kionjo cha video jinsi mamake na dadake walimkabidhi zawadi hio iliyokuwa imefichwa ndani ya shada la maua.

Baada ya kuichomoa, alipigwa na butwaa kupata ni simu aina ya iPhone 15 pro max yenye uwezo wa kubeba video na nyimbo kwa hadi 1TB.

Kinuthia alishindwa kuzuia machozi yake ya furaha na kusema kwamba zawadi ya simu ya iPhone 5 ndicho kitu ambacho amekuwa akililia ngoa kwa muda mrefu.

“Weeh guys lemme tell you my family did it  ️Aki waah hata nakosa maneno️  Dada yangu na mama yangu walinishangaza kwa zawadi yangu ya ndoto️Am such a proud girl kuwa na wanafamilia kama hao ️Asante Mama, Asante Maureen ,Asante zaituni,” Kinuthia alisema, akijisisitizia kuwa yeye ni msichana.

“Weeh Leo ni Leo 😩❤️Mwishowe nilipata hisia ya mshangao 😩❤️Familia yangu ilifanya muujiza. MTUMIAJI mpya kabisa wa iPhone 15 pro max 1TB mwaka wa 254️ Asante kwa mama na dada yangu kwa mshangao huu mzuri na mzuri   ️Nina furaha sana hata sina maneno ya kuelezea au kuelezea furaha yangu,” aliongeza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved