Showmax yazindua msururu wa kwanza wa makala Kenya 'Nilichoma'

Msururu huu wa sehemu 10 unaangazia watu mashuhuri wa Kenya ambao walijizolea utajiri wa ghafla na wakaupoteza wote.

Muhtasari

• Nilichoma ni mkusanyiko wa ndoto hizi, zinazosimuliwa na watu ambao tumekua nao nakuotakuwa. Watu hawa ama walirithi, walishinda, au walitunukiwa pesa nyingi zaidi ya ndoto zao. 

• Lakini ndoto hizi ziligeuka kuwa ndoto mbaya kwa matumizi mengi zaidi, na mara zilipogonga mwamba, kilichobaki ni masomo magumu tu yakujifunza.

Showmax Original series Nilichoma
Showmax Original series Nilichoma
Image: Showmax

Kampuni kubwa ya upeperushaji mtandaoni kutoka Afrika ya Showmax imezindua msururu wa kwanza kabisa wa makala nchini Kenya, "Nilichoma," iliyoonyeshwa kwa mara ya kwanza Mei 28.

Msururu huu wa sehemu 10 unaangazia watu mashuhuri wa Kenya ambao walijizolea utajiri wa ghafla na wakaupoteza wote, na hivyo kutoa uchunguzi wa kuvutia wa mali na asili yake ya kupita.

"Hadithi ya kuanza chini, na kuangukia tu katika utajiri mkubwa, ni ndoto inayozungumziwa na wanadamu. Hata hivyo, kuanguka kutoka juu hadi chini kunako ambatana na hali hiyo ni jinamizi tunaloogopa," anasema mtayarishaji Ahmed Deen ("Midlife Crisis")."

Nilichoma ni mkusanyiko wa ndoto hizi, zinazosimuliwa na watu ambao tumekua nao nakuotakuwa. Watu hawa ama walirithi, walishinda, au walitunukiwa pesa nyingi zaidi ya ndoto zao. Lakini ndoto hizi ziligeuka kuwa ndoto mbaya kwa matumizi mengi zaidi, na mara zilipogonga mwamba, kilichobaki ni masomo magumu tu yakujifunza.

"Nilichoma inawakilisha ndoto za Wakenya kutoka tabaka zote za maisha. Msururu huu unanasa matukio mbichi ya kihisia ambayo huruhusu watazamaji kutafakari na kuangalia ndani ya mioyo yao kupitia wanaume na wanawake kwenye skrini," anaongeza mtayarishaji mwenza Isaya Evans.

"Nilichoma" inatoa uzoefu wakihisia wa kina kupitia hadithi 13 tofauti, ikichanganya masimulizi ya kibinafsi, mahojiano, picha na video kwenye kumbukumbu, na uigizaji upya unaoonyesha kuinuka, kuanguka, na mageuzi ya baadaye ya watu hawa.

Makala haya yanajumuisha nyota wa kriketi Maurice Odumbe, mchekeshaji JB Masanduku, David Ogot (mtoto wa mwandishi mashuhuri na mwanasiasa Grace Ogot), milionea wa zamani wa Samburu Gabriel Lengishili, na wengineo.

Deenna Evans wanashirikia na kutengeneza makala haya chini ya Café Luna Films, inayojulikana kwa kazi yao ya "The Real Housewives of Nairobi," "The Girl with the Yellow jumper," "Shimoni," "Igiza," na "Ayaanle."

"Nilichoma" inaungana na vipindi halisi vya Showmax vingine vitatu vya Kenya iliyoonyeshwa kwa mara ya kwanza mwezi Mei, kuashiria uzinduzi upya rasmi wa mpeperushaji huyo nchini Kenya.

Vipindi hivyo vinajumuisha "The Real Housewives of Nairobi" msimu wa 2 unaotarajiwa sana, tamthilia mpya "Untying Kantai" kutoka Philit Productions, na mfululizo mpya wa romcom "Big Girl Small World" kutoka kwa Nick Mutuma na Kevin Njue.

Tazama msururu huu unaoibua mawazo kwenye Showmax pekee: Jisajili kwenye Showmax.com kutumia M-Pesa.

Showmax inatoa anuwai ya chaguzi za usajili za bei nafuu:

  • Showmax Entertainment – ​​KES 650: Tazama vipindi Asilia vya Showmax, misururu ya kimataifa na ya ndani, filamu na vipindi vya watoto kwenye TV na vifaa vya mkononi.
  • Showmax Entertainment Mobile – KES 300: Tazama kwenye kifaa kimoja cha mkononi pekee.
  • Showmax Premier League - KES 500: Tazama ligi Kuu Moja kwa Moja kutoka kwa SuperSport, pamoja na ufikiaji wa maudhui yote kwenye kifaa chako cha mkononi.
  • Chaguo za Bundle:
  • Burudani ya Showmax + Ligi Kuu - KES 1000.
  • Showmax Entertainment Mobile + Ligi Kuu - KES 700