Ujumbe mtamu wa Museveni kwa mkewe anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa

Katika ujumbe wake mzuri, Museveni alimuelezea Mke wa Rais kama 'rafiki aliyepewa na Mungu'.

Muhtasari
  • Museveni kupitia akaunti yake rasmi ya  X alisherehekea mke wake wa miaka 51 huku akitimiza miaka 76.
RAIS WA UGANDA TOWERI MUSEVENI NA MKEWE JANET
Image: MUSEVENI/ X

Rais wa Uganda Yoweri Museveni Jumatatu alisherehekea siku ya kuzaliwa ya mkewe Janet.

Museveni kupitia akaunti yake rasmi ya  X alisherehekea mke wake wa miaka 51 huku akitimiza miaka 76.

Katika ujumbe wake mzuri, Museveni alimuelezea Mke wa Rais kama 'rafiki aliyepewa na Mungu'.

Alisema Janet, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Museveni Incorporated, alichukua jukumu muhimu katika maisha yake ya ujana.

"Mkuu wa kikundi cha Museveni, mama, bibi, mwenzangu niliyepewa na Mungu wa karibu miaka 51, mke wangu mpendwa, Maama Janet Museveni, ametimiza miaka 76," alisema.

"Bwana asifiwe aliyetusaidia kuvuka changamoto nyingi na kutupa baraka nyingi," alisema.

Museveni alisema kuwa jukumu la kipekee la Mama Janet katika hadithi ya familia yao lilitoka kati ya 1981 na 1986 walipolazimika kumpeleka uhamishoni pamoja na watoto wao wachanga.

Wanajumuisha Muhoozi, Natasha, Patience na Diana wakati Muhoozi alikuwa na umri wa miaka sita tu wakati Diana alikuwa na miezi sita.