logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bosi wa Mavin Records Don Jazzy, 41, afunguka kwanini hajaoa

Don Jazzy alikubali hili, na alikiri kwamba anapenda wanawake, na hiyo inaelezea kwa nini bado hajaoa tena.

image
na Davis Ojiambo

Burudani27 June 2024 - 06:17

Muhtasari


  • β€’ "Mara tu unapofungua ukurasa wowote wa warembo kwenye instagram kitu cha kwanza utaona ni "unafuatiwa na don jazzy". Mwanaume huyo yuko kila mahali πŸ˜‚,” aliandika.

Mtayarishaji maarufu wa muziki, Don Jazzy, hatimaye amefichua kwa nini hajaoa, huku akimjibu mwanamtandao ambaye aligundua kuwa anafuatilia kwa bidii watu kadhaa kwenye Instagram.

Itakumbukwa kuwa bosi huyo wa Mavin Records aliwahi kuoa kabla ya ndoa yake kugonga mwamba.

Mwanamtandao mmoja alienda kwenye Twitter kushiriki maoni yake kuhusu Don Jazzy.

Mwanamtandao huyo anayejulikana kwa jina la @UGBEDE__ alitoa maoni kwamba kila anapofungua ukurasa wowote wa Instagram wa mrembo, mtu mashuhuri wa kwanza kuona akimfuata mwanamitindo huyo atakuwa Don Jazzy.

"Mara tu unapofungua ukurasa wowote wa warembo kwenye instagram kitu cha kwanza utaona ni "unafuatiwa na don jazzy". Mwanaume huyo yuko kila mahali πŸ˜‚,” aliandika.

Don Jazzy alikubali hili, na alikiri kwamba anapenda wanawake, na hiyo inaelezea kwa nini bado hajaoa tena.

“Mimi napenda mabinti wazuri na ndio maana sijawahi tulia kwenye ndoa,” Don Jazzy alijibu.

Mwaka 2022, Don Jazzy alidaiwa kuwa miongoni mwa watu waliokereka baada ya msanii Rihanna kuweka wazi kwamba alikuwa anatarajia mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake ASAP Rocky.

Inadaiwa kwamba Jazzy alikuwa kwa muda mrefu akimfuatilia Rihanna kwa lengo la kumuoa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved