logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize ampongeza Burna Boy kwa kujaza watu 80k kwenye uwanja wa tamasha nchini UK

"Hongera bingwa, hii inatisha sana. Hivi, hii inawezekanaje?” Harmonize alijiuliza.

image
na Davis Ojiambo

Burudani30 June 2024 - 12:14

Muhtasari


  • • Harmonize alichapisha klipu kutoka kwa tamasha hilo na kumhongera Burna Boy kwa hatua hiyo kubwa ya kujaza uwanja kwa mashabiki 80k katika ardhi ya ughaib
Burna Boy na Harmonize

Kwa mara nyingine tena Harmonize ameonyesha kudumisha urafiki wake na staa mkubwa wa Afrobeats, Burna Boy.

Mwishoni mwa juma, Burna Boy alikuwa na tamasha kubwa nchini Uingereza ambapo kwa mara nyingine aliweka historia kwa kuvutia mashabiki Zaidi la elfu 80 kujaza uwanja huo.

Harmonize alichapisha klipu kutoka kwa tamasha hilo na kumhongera Burna Boy kwa hatua hiyo kubwa ya kujaza uwanja kwa mashabiki 80k katika ardhi ya ughaibuni.

Harmonize kwa utani alisema kwamba Burna Boy amekua na kuwa staa mkubwa kiasi kwamba hata yeye sasa ameanza kujihisi kwamba hamjui tena kwani Burna Boy wa sasa ni tofauti na yule wa miaka 6 nyuma wakifanya naye Kolabo ya Kainame, ambayo pia walimshirikisha bosi wake kipindi hicho, Diamond Platnuma.

“Binafsi naweza nikasema simjui Burna Boy tena kwa sababu yeye si yule Oluwa nilikuwa namjua. Hongera bingwa, hii inatisha sana. Hivi, hii inawezekanaje?” Harmonize alijiuliza.

Picha na video kutoka kwa tamasha hio lililofanyika usiku wa Jumamosi zilionyesha uwanja wa London wenye uwezo wa kusheheni mashabiki elfu 80 ukiwa umefurika huku mashabiki wakiserebuka kwa mbwembwe.

Hata hivyo, baadhi walihoji kwa nini Harmonize hakumhongera rafiki yake Rayvanny ambaye siku moja iliyopita alikuwa na tamasha kuu nchini Albania ambapo pia alijaza uwanja, lakini akawa wa haraka kumhongera Burna Boy.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved