logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ciru Muriuki asherehekea siku ya kuzaliwa ya marehemu Charles Ouda miezi 5 baada ya kufa

"Heri ya siku ya kuzaliwa, mpenzi wangu wa milele," Ciru alinukuu.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 July 2024 - 08:04

Muhtasari


  • • Hii bila shaka ni moja ya ishara na dalili zinazoashiria jinsi Ciru alikuwa amewekeza hisia zake za mapenzi kwa Ouda kabla ya mkono bahili wa kifo kuzua utengano wao.
  • • Itakumbukwa katika mahojiano ya hivi majuzi, Ciru Muriuki alitaja kuwa usaidizi wa mamake umemsaidia kukabiliana na msiba wa ghafla wa mpenzi wake.
CHARLES OUDA NA CIRU MURIUKI

Aliyekuwa mtangazaji wa TV Ciru Muriuki ameendeleza kudumisha nadhiri ya moyoni mwake kutomsahau katu mpenzi wake, marehemu muigizaji Charles Ouda.

Hili limedhihirika kwa mara nyingine baada ya Muriuki kuwakumbusha mashabiki wake na kwamba wiki hii ni moja ya siku maalum katika maisha yake kwani ndiyo wakati marehemu Ouda alipozaliwa.

Ouda ambaye alifariki mapema mwezi Februari mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha walikuwa kwenye mapenzi na Muriuki kwa muda.

Ciru Muriuki alipeleka kwenye kurasa za mitandao ya kijamii kufahamisha ulimwengu kwamba licha ya Ouda kutangulia mbele za haki, bado atasalia kuwa mpenzi wake milele, na atazidi kumuenzi.

Alimuandikia ujumbe marehemu Ouda akimtambua kama mpenzi wake wa milele na kuisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

"Heri ya siku ya kuzaliwa, mpenzi wangu wa milele," Ciru alinukuu.

Hii bila shaka ni moja ya ishara na dalili zinazoashiria jinsi Ciru alikuwa amewekeza hisia zake za mapenzi kwa Ouda kabla ya mkono bahili wa kifo kuzua utengano wao.

Itakumbukwa katika mahojiano ya hivi majuzi, Ciru Muriuki alitaja kuwa usaidizi wa mamake umemsaidia kukabiliana na msiba wa ghafla wa mpenzi wake.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Ciru alishiriki picha yake na mamake, akimsifu kama malkia ambaye alimsaidia kupata nafasi yake katika miezi iliyofuata kifo cha mwenzi wake.

Akinukuu picha hiyo, Mshauri wa Milenia alianza kwa kukiri nguvu na uzuri wa mama yake:

“Kwa kweli mimi ni binti wa mama yangu. Ninaweza tu kutumaini kuwa nusu ya mwanamke alivyo.” Aliongeza, "Nisingeweza kumaliza miezi 4 iliyopita bila yeye ... malkia."

Ouda alifariki akiwa na umri wa miaka 38 na miezi 5 baadae, chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi kwa mashabiki wa kazi zake za Sanaa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved