Mwanadada amuagiza Larry Madowo amuoe kwa lugha ya matusi, ajibu

“Mlisema huu mwaka ni wa mwaka wa kuforci?” Madowo alionekana kushangaa.

Muhtasari

•Mwanadada huyo ambaye hakutambulishwa alionekana kutumia lugha isiyo ya adabu kufanya ombi hilo lisilo la kawaida.

•Mwanahabari huyo wa zamani wa NTV alielezea mshangao wake akishangaa ikiwa mwaka huu ni wa kulazimisha mambo.

Larry Madowo,
Larry Madowo,
Image: X// LARRY MADOWO

Mwanahabari wa kimataifa wa Kenya Larry Madowo alionekana kushangazwa baada ya mtumiaji wa mitandao ya kijamii kumwandikia ujumbe akimuomba amuoe.

Katika ujumbe ambao mwanahabari huyo wa CNN alichapisha kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter, mtumiaji huyo wa mitandao ya kijamii ambaye hakutambulishwa alionekana kutumia lugha isiyo ya adabu kufanya ombi hilo lisilo la kawaida.

“Larry si unioe Ngamia hii,” mtumiaji huyo wa mtandao wa kijamii aliandika.

Katika majibu yake, mwanahabari huyo wa zamani wa NTV na KTN alielezea mshangao wake akishangaa ikiwa mwaka huu ni wa kulazimisha mambo.

“Mlisema huu mwaka ni wa mwaka wa kuforci?” Madowo alionekana kushangaa.

Mapema mwaka huu, mwanahabari huyo mwenye umri wa miaka 36 alionekana kuthibitisha kwamba bado yeye ni kapera na hajaoa.

Madowo ambaye kwa sasa anafanya kazi katika shirika la habari la CNN alisema kuwa bado ana muda wa kuoa kufuatia habari za mfanyabiashara tajiri Rupert Murdoch kufunga ndoa akiwa na umri wa miaka 92.

Madowo alichapisha screenshot ya kichwa cha habari cha ndoa ya Bw Murdoch na kunukuu, "Bado nina wakati."

Huenda huu ulikuwa uthibitisho kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa NTV bado hajaoa licha ya kuhusishwa kimapenzi na mwanahabari mwenzake Edith Kimani.

Kwa muda mrefu, Wakenya wamekuwa wakidhani kwamba wawili hao wanachumbiana, kufuatia matendo yao ya wazi kwenye mitandao ya kijamii na matukio yao mazuri ya pamoja ambayo mara nyingi huwa wanashiriki hadharani.

Kuelekea mwishoni mwa mwezi Januari, Madowo aliamua kuwafanya mashabiki kukisia zaidi kwa ku-share post ambayo ilizidisha tetesi hizo kuwa yeye na Edith ni zaidi ya marafiki wa karibu.

Picha hiyo zuri iliambatana na nukuu fupi na tamu iliyosomeka, "Ikiwa sio hivi, sitaki📸 @gathigesest."

Na alichokuwa anakitaka Larry, ndicho alichokipata, kuzungumziwa. Chapisho hilo liliibua hisia mseto kutoka kwa mashabiki wake ambao waliamua kusherehekea 'uhusiano' kati ya nyota hao wawili wa habari.

Mapema mwaka jana, Edith alishiriki picha nzuri iliyoonyesha akimbusu Larry kwenye shavu lake na ujumbe mzuri kuhusu upendo wao kwa kila mmoja.

Edith alinukuu tukio hili,"Mwaka mpya. Same me. Bili sawa. Same love.@larrymadowo amechange wallet lakini, kwa hivyo matumizi mpya."

Wawili hao kwa muda mrefu wamekuwa wakidhaniwa kuwa wapenzi lakini hawakuwahi kuifanya rasmi.