logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ringtone atoa wito watu kuwatembelea majeruhi wa waandamano hospitalini

Alieleza sababu yake kuu ya kuwahimiza watumiaji wa mtandao kuwatembelea waandamanaji waliojeruhiwa.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 July 2024 - 13:57

Muhtasari


  • •Alieleza sababu yake kuu ya kuwahimiza watumiaji wa mtandao kuwatembelea waandamanaji waliojeruhiwa.
  • •Alieleza kuwa watu ambao waliojeuriwa wakati wa maandamano wanaitaji msaada wa kila mtu.

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Ringtone Apoko ametuma ujumbe kwa watumiaji wa mtandao na wabunge kuwatembelea waandamanaji waliojeruhiwa katika eneo lao wakati wa maandamano.

Msanii huyo wa nyimbo za injili aliwatia moyo  waandamanaji waliojeruhiwa alipokuwa akitoa msaada wake alipowatembelea hospitalini baadhi ya waliojeuriwa. 

“Unajua unaweza kuta kuna kijana alitoka nyumbani vizuri na kuingia mitaani kupigania haki yake na mustakabali mwema akipiga kelele ‘kataa’ na sasa utakuta yuko peke yake hapa hospitalini."

Kutokana na hilo, unajua ni rahisi sana kwa vijana hawa kukata tamaa,”alisema.

Alieleza sababu yake kuu ya kuwahimiza watumiaji wa mtandao na watu wote kuwatembelea waandamanaji waliojeruhiwa ni kwamba watawahitaji wakati mwingine wajitokeze kwa jambo kama hilo.

”Wakati ujao kitu kikitokea na tunaomba vijana wajitokeze wengi wao wataambiwa, 'unakumbuka ulipoumia ulikuwa peke yako hapa, unaweza kukuta kuna mgonjwa ambaye tangu asubuhi hadi sasa' ajakuwa na wageni  na hatutaki hilo lifanyike.”

“Ningependa kuwatia moyo na pia kila mtu ambaye alikuwa kwenye maandamano, watu hawa wanakuhitaji sasa kuliko hapo awali. Sasa kwa kuwa wako peke yao, wanatuhitaji,” alisema.

Rightone alimwomba Rais kuwapinga kalamu mawaziri ambao awastahili kuwa kwa ofisi na pia kupunguza wizara zingine hili kupunguza pesa zinazotumika.

Haya yanajiri baada ya tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR)kuweka idadi ya waliofariki kutokana na maandamano kote nchini kuwa 39 na waliojeruhiwa kuwa 361.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved