logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Cassypool asema sababu ya kupeana mshahara akiwa gavana

Cassypool pia alimpongeza Charlene Ruto kwa kutoka katika eneo lake la comfort zone na kusikiliza masuala ya Gen Z.

image
na Davis Ojiambo

Burudani05 July 2024 - 12:59

Muhtasari


  • •Cassypool pia alimpongeza Charlene Ruto kwa kutoka katika eneo lake la comfort zone na kusikiliza masuala ya Gen Z.
  • •Alisema kuwa atatoa mshahara wake kwa watu kwa sababu anataka kuonesha mfano kama mmoja wa watu bora waliowahi kuwaongoza watu bila kuchukua pesa.
Cassypool

CassyPool  alisema angewania ugavana 2027.Alisema kuwa atatoa mshahara wake kwa watu kwa sababu anataka kuonesha mfano kama mmoja wa watu bora waliowahi kuwaongoza watu bila kuchukua pesa.

Alisema kuwa kazi yake itakuwa ya kuwatumikia watu waliomchagua, kwani yeye hajali tu juu ya mshahara.

“Nikikua Governor salary yangu iende kwa wananchi wasaidike na hiyo salary yangu naisema kwa macho yangu mshahara iende kwa wananchi of course napewa allowance hizi zingine ndogo ndogo hizi za gari za nyumba mimi niko huko kuwafanyia kazi.

Wanataka hii pesa yote ya kazi gani mimi ni niwafanyie kazi miaka tano niende nyumbani.” Cassypool alisema.

Cassypool pia alimpongeza Charlene Ruto kwa kutoka katika eneo lake la comfort zone na kusikiliza masuala ya Gen Z.

“Nataka kumpongeza mdogo wangu mtoto wa kwanza kwa rais ambaye ana nidhamu, anajituma ametoka kwenye comfort zone yake kwa sababu ameamua aje asikize issues zenye zinakabidhi Gen Z’s wenzake.” Cassypool alisema.

Hata hivyo alimtetea Charlene Ruto kutoka kwa wakosoaji wa mtandaoni akisema wanapaswa kushukuru mbingu.

Alieleza kwamba kwa mara moja nchi ina mtoto wa Rais wa Kenya ambaye yuko tayari kufanya kazi na vijana na umma kuona mabadiliko nchini licha ya kuwa yuko vizuri katika nafasi yake.

“Mimi namshukuru sana mtoto wa rais ambaye haendi kuchukua risasi kupiga nazo ndege tuko na mtoto wa rais ambaye hakunywi madawa, ambaye anahishi kanisani anaomba mungu.

Charlene Ruto amekua kipao mbele kama miaka mbili hivi sasa.

Tuko na mtoto wa rais ambaye amefanya vitu vingi zenye hazijawahi historia ya Kenya na watoto wa rais. Weka heshima.” Cassypool alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved