logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Octopizzo atuma ujumbe kwa Rais Ruto

Alieleza zaidi kuwa alikuwa ametengeneza video akimweleza rais njia za kupunguza maandamano hayo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani08 July 2024 - 12:50

Muhtasari


  • • Mamia ya Wakenya walikusanyika katika bustani ya Uhuru kwa tamasha la ShuGenz kuwaenzi wenzao waliouawa katika maandamano ya hivi majuzi dhidi ya serikali.
  • • Alieleza zaidi kuwa alikuwa ametengeneza video akimweleza rais njia za kupunguza maandamano hayo.
  • • Octopizzo alieleza kuwa kile wanamtandao wengi walikuwa wakilalamikia, akitaja kuwa sio watu wanaoishi Nairobi pekee ambao hawapendezwi na serikali ya sasa, bali kila kaunti.
Octopizzo,

Mwanamuziki wa Kenya Octopizzo ameeleza maoni yake kuhusu kile anachoamini kuwa kinaweza kuwa suluhu la kuzuia maandamano.

Octopizzo alishiriki ujumbe wake kwa rais akiwa Uhuru Park wakati wa tamasha ya kuwaenzi watu waliokufa wakati wa maandamano.

Octopizzo alianza kwa kueleza kile wanamtandao wengi walikuwa wakilalamikia, akitaja kuwa sio watu wanaoishi Nairobi pekee ambao hawapendezwi na serikali ya sasa, bali kila kaunti.

"Kwangu mimi ni ya kibinafsi sana. Sikujangi huku hivi hivi. Natamani tungeweza kufanya onyesho hili kila kaunti. Ndio watu waone sio Nairobi pekee imechoka. Kila mtu amechoka,” alishiriki na SPM Buzz.

Alieleza zaidi kuwa alikuwa ametengeneza video akimweleza rais njia za kupunguza maandamano hayo.

”Prezzo huku nje rada chafu. Nilimwambia vile anaweza kuokoa doh. Hizi ni mawazo tuko nazo. Aende acheki hio video."

"Ata jifunze vitu tatu, nne venye ata change situation. But the most important thing naweza ambia president, corruption ndio inatumeshea,” Octopizzo alisema.

Mamia ya Wakenya walikusanyika katika bustani hiyo kwa tamasha la ShuGenz kuwaenzi wenzao waliouawa katika maandamano ya hivi majuzi dhidi ya serikali.

 Maandamano hayo yalizuka mwezi Juni kuhusu mapendekezo ya nyongeza ya ushuru na kutaka Rais William Ruto ajiuzulu.

Katika bustani ya Uhuru, vijana walishikilia mabango yenye maandishi “RIP Comrades” na “Tunaahidi tutaendelea kupigana.”

Umati huo uliimba kauli mbiu dhidi ya ya utawala wa sasa huku baadhi wakipiga misalaba ardhini.

Muda wa tamasha ulikuwa na umuhimu,kwan uliadhimisha Siku ya Saba Saba, siku ya kihistoria mwaka 1990 wakati maandamano yaliposababisha kurejea kwa demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved