logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Dem Wa Facebook aonyesha nyumba anayowajengea wazazi wake

Pia alifafanua kuwa sababu iliyomfanya aamue kuwafahamisha mashabiki wake kuwa anajenga nyumba hiyo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 July 2024 - 09:37

Muhtasari


  • •Mtayarishi wa Maudhui nchini Kenya Dem Wa Facebook ameonyesha nyumba yenye vyumba vitatu anayowajengea wazazi wake.
  • •Pia alifafanua kuwa sababu iliyomfanya aamue kuwafahamisha mashabiki wake kuwa anajenga nyumba hiyo.
  • •Dem Wa Facebook aliendelea kusema kwamba alichagua kuwajengea wazazi wake nyumba hiyo si kwa sababu ya upendo wake kwao tu bali kwa sababu yeye ndiye mlezi na anapaswa kuwa mfano mzuri kwa wengine kufuata.

Mtayarishaji wa maudhui alichapisha picha za nyumba inayokaribia kukamilika, ambayo iko kwenye hatua ya kuweka paa, kwenye mitandao ya kijamii.

Dem Wa Facebook ambaye aliweka video ya nyumba hiyo ambayo bado inaendelea kujegwa kwenye chaneli yake ya YouTube.

Alimshukuru Mungu kwa hatua aliyofikia na kwa upande huo huo akikiri na kutoa pongezi kwa wanawake wote ambao wamekuwa wakimuunga mkono na kumtia moyo kila wakati.

“Mambo ya mungu na bidii, nimeamua kujenga wazazi wangu 3bedroom house ndio wakae vizuri wakiwa hai bado."

"I have genuine fans, thanks a lot my fans pia mumenisupport sana the power of ladies may God bless you hata wao ndio wamenimotivate nikuje home niwaonyeshe one two huku home.” Dem Wa Facebooks alisema

Dem Wa Facebook aliendelea kusema kwamba alichagua kuwajengea wazazi wake nyumba hiyo si kwa sababu ya upendo wake kwao tu bali kwa sababu yeye ndiye mlezi na anapaswa kuwa mfano mzuri kwa wengine kufuata.

Hii nyumba nimejenga 3 months mahali tumefika ni process ya kueka mabati….na my wish ni by December nataka ikuwe ready tufungue hii Nyumba….mimi ndio breadwinner kwetu na lazima nitengeneze Nyumbani.” Dem Wa Facebook alisema.

Kwa kuzingatia video aliyoiweka kwenye YouTube nyumba hiyo ni pana sana na kila sehemu ina madhumuni yake, inakaribia kukamilika kwani ina vitu vichache tu vilivyosalia ambavyo ni madirisha, plasta na umeme.

Pia alifafanua kuwa sababu iliyomfanya aamue kuwafahamisha mashabiki wake kuwa anajenga nyumba hiyo yenye vyumba itatu.

Alisema ni kutokana na baadhi ya watu mtandaoni  kutaka kujua anachofanya na pesa anazozipata jambo ambalo kwa sasa amelitolea ufafanuzi kuonyesha kile ambacho amekuwa akifanyia kazi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved