logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Willy Paul atangaza mpango wa kuanza kuingia kwenye DM za warembo kuwapa kazi

“Wewe ni mwanamke mrembo sana? Model type? Sawa, nitarajie kwenye DM yako mimi mwenyewe' alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani11 July 2024 - 08:01

Muhtasari


  • • Msanii huyo anayezidi kutamba kwa albamu ya Beyond Gifted alisema kwamba atakuwa anaingia kwenye faragha za mabinti hao kuwapa kazi .
WILLY PAUL

Msanii Willy Paul ambaye wiki chache zilizopita alidai kuhamisha Ujerumani ametangaza kuwa ana mpango wa kuwapa wasichana warembo kupita kiasi kazi kwenye DMs zao.

Pozee, kama anavyojiita alichapisha ujumbe huo kwenye Instastory yake akisema kwamba msichana yeyote ambaye ni mrembo kupindukia na anatumia mtandao wa Instagram, asishangae atakapomuona kwenye DM yake.

Msanii huyo anayezidi kutamba kwa albamu ya Beyond Gifted alisema kwamba atakuwa anaingia kwenye faragha za mabinti hao kuwapa kazi ambazo hata hivyo hakuweka wazi ni kazi za aina gani.

“Wewe ni mwanamke mrembo sana? Model type? Sawa, nitarajie kwenye DM yako mimi mwenyewe. Hivyo, ukiniona ninakuomba namba yako usishangae, niko na kazi kwako,” Pozee alichapisha.

Pozee amefunguka kuwa na mpango wa kuingia kwenye DM za warembo, miezi kadhaa baada ya baadhi ya watu kuvujisha mazungumzo kwenye DM ambayo yalidaiwa kuwa ya msanii huyo kwa warembo mbalimbali.

Licha ya kuweka wazi kwamba ni suala la kazi tu litamfanya kuwafuata warembo wa sampuli anayoitaka kwenye DM, baadhi katika upande wa kutoa maoni walihisi ni ajenda nyingine ambayo analenga.

Haya hapa ni baadhi ya maoni;

“Watu sii wajinga bwana 😂😂😂 one lege... anguka nayo 😂😂” @wangubest.

“Bora nisikuone kwa Dm ya Dem yangu ,😢nitaanguka nawewe😢” @boilingpoint_ke

“Wewee willy nakuona umeanz kujitetea apa kuna tea tunaanguka nayo BNN leta hio tea😂😂😂😂” @zuhuraswaleh59

“We tunakujua.... unataka kuanguka nao😂😂😂” @whoza.boy5

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved