Mchekeshaji Mannerson Oduor Ochieng, anayejulikana pia kama Akuku Danger bado anaendelea kuimarika katika uhusiano wake na mwigizaji Sandra Dacha.
Wapenzi hao wawili wamefanikiwa katika uhusiano wao, lakini pia wamethibitisha umoja wao kwa miaka ambayo wamekuwa pamoja.
Hapo awali Akuku Danger akuwa ameweka mahusiano yake hadharani, hadi alipokutana na Sandra Dacha.
Walianza kama marafiki wazuri, ambao mara nyingi walitayarisha maudhui pamoja na kuchapisha kwenye mitandao ya kijamii.
Katika mahojiano ya hivi majuzi kwenye Obinna TV, Akuku Danger alifichua kwamba Sandra Dacha ndiye aliyemkatia.
”Sandra ndio alinitia kwa matanga ya Othuol,” Akuku alisema.
Tunafahamu vyema kwamba Akuku Danger anaishi na sickle cell anaemia na alikuwa mgonjwa sana miezi kadhaa iliyopita.
Pia kumshukuru kwa kusimama naye wakati alikuwa akimhudumia hospitalini.
Sandra Dacha ni miongoni mwa watu ambao wamesimama karibu naye hio ikiwa miongoni mwa mambo anayopenda kuhusu Sandra.
"Kupata mtu ambaye anaweza kuwa karibu nawe katika hali ngumu na mbaya sio rahisi. Sandra alikuwepo kwa ajili yangu wakati wote."
"Akinihudumia hospitalini na kuhakikisha kila kitu kiko sawa. Ninampenda na kumthamini kwa hilo. Watu wengi wangeondoka. Tumekuwa pamoja kwa miezi 7 na ndio ni wangu,” alikiri.