Eric omondi atoa onyo jipya kwa wabunge baada ya kuvunjwa baraza la mawaziri
Mcheshi Eric Omondi alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa maandamano dhidi ya serikali. Mkejeli huyo, ambaye amekuwa katika tasnia ya burudani kwa zaidi ya miaka 17.
Aliamua kuwa atasaidia kupambana na viongozi wafisadi serikalini na kuwasaidia Wakenya wasiojiweza.
Bidii ya Eric imechochewa na ukweli kwamba Wakenya pia walimuunga mkono wakati wake kama mcheshi.
Alisema kuwa njia pekee ya kurudisha fadhila hiyo ni kuwasaidia katika kupambana na viongozi wafisadi.
Hivi majuzi, maandamano ya kupinga mswada wa fedha yalizaa matunda.
Ingawa kukosekana kwa Eric Omondi kulionekana wazi, Gen Z walimwakilisha vyema huku akiwataka wapigane.
Kwa bahati mbaya, ni katika kipindi hiki ambapo Eric alipoteza nduguye wa damu Fred Omondi katika ajali ya barabarani.
Maandamano hayo yalifaulu! Lakini Eric Omondi hajamalizana na serikali.
Akiongea katika mahojiano ya hivi majuzi, Eric Omondi alithibitisha kuwa yuko tayari kuwafuata wabunge waliopiga kura ya ‘ndio’ kwa mswada wa fedha.
“Nataka niwaahidi, kila mbunge aliyepiga kura ya ‘ndiyo’ tuna picha zao, tuna majina yao, tuna majimbo yao. Tunaenda kusambaza majina yao. Tutaziimba kama wimbo wa taifa.”
Eric alitoa ahadi hiyo kuwakumbusha Wakenya kuhusu wabunge hao na kuhakikisha kwamba hawapigiwi kura baada ya IEBC kufanya mageuzi.
”Wale walivote yes hawatafika 2027, tutawarecall wote. Kwanza hao waliapologize ndio tunaanza nao,” Eric aliahidi.